Featured Kitaifa

TANZANIA KUENDELEA KUBUNI MAENEO MAPYA YA URITHI WA DUNIA 

Written by mzalendoeditor
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana ,akifungua mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya utekelezaji wa mkataba wa UNESCO wa mwaka 1972 maadhimisho yanayoendea mkoani Arusha.
BAADHI ya wataalamu wa masuala ya urithi wa Dunia wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya utekelezaji wa mkataba wa UNESCO wa urithi wa Dunia unaoendelea mkoani Arusha.
MKUU wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya urithi wa ulimwegu Afrika kutoka UNESCO Mohamed Mohamed akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo.
PICHA ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana pamoja na baadhi ya wataalamu kutoka nchi mbalimbali Duniani.
……………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

WAZIRI  wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana amesema kuwa Tanzania itaendelea kubuni maeneo mapya ambayo yatahifadhiwa kama urithi wa Dunia kwaajili ya kuongeza mazao ya utalii pamoja na kuhifadhi kwa vizazi vya Sasa na baadae.

Dkt Chana aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya  utekelezaji wa mkataba mkataba wa UNESCO wa urithi wa kidunia wa kitamaduni na kimazingira mkataba ulioletwa mwaka 1972 na kuridhiwa na Tanzania mwaka 1977 unaendea mkoani Arusha.
Alieleza kuwa maeneo ya urithi wa Dunia Kuna namna yake ya kuyatunza lakini ili kutambuw kuwa eneo hili ni urithi Kuna  vipo ambavyo vinahitaji wataalamu wabobezi katika kuyatambua maeneo yote mapya kwaajili ya kuhifadhi uridhi wa Dunia.
“Tanzania tuna maeneo yasiyopungua 7 ya urithi wa Dunia na katika Afrika tunaongoza kwa kuwa na maeneo mengi ya urithi lakini bado wakati upo tuendelee kubuni maeneo mengine ya utalii ambayo tutayahifadhi Kama urithi wa Dunia,” Alisema Balozi Dkt Chana
“Mkutano huu umelenga kuendelea kutoa elimu ni namna gani tunaweza  kuelewa masuala haya ya urithi wa Dunia ambapo Kuna mkataba wa Dunia ambao sisi Tanzania tumeusaini tangu mwaka 1977 na nilazima tuelewe ni kwa namna gani tunatekeleza  lakini pia bado tunahitaji maeneo mengine mazuri ya yatakayotambulika kama urithi wa kidunia,” Alisema Dkt Chana.
“Tunaposema kutoa elimu pia kwasasa tumelenga suala la usawa wa kijinsia katika eneo hili la uridlthi wa Dunia kwani watu wengi wanaosomea masuala haya ni wanaume hivyo tumeona ni muhimu pia kuangalia ni namna gani tunashirikisha wanawake,”Alieleza.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya urithi wa ulimwegu Afrika kutoka UNESCO Mohamed Mohamed alisema mkataba huo wa mwaka 1972 mwaka huu umetimiza miaka 50 hivyo wanasherekea  huku wakiangalia miaka 50 ijayo watafanya nini katika kutekeleza mkataba huo.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuangalia katika masuala ya elimu kwani pamoja na kwamba wamefikisha miaka 50 Afrika bado Ina matatizo katika kutekeleza mkataba huo ikiwemo kutokuwepo kwa wataalamu wanawake pamoja na vijana ambapo wataondoka na maadhimio ambayo UNESCO na kuweka mikakati ya miaka 50 ijayo.
Hata hivyo zaidi ya wataalamu 50 kutoka nchi mbalimbali Duniani wameshiriki  katika mkutano huo ulioenda  sambamba na maadhisho hayo ambapo Afrika Ina urithi wa kidunia wa asili na kitamaduni 98 sawa na asilimia 8.5, nchi za Uarabuni zikiwa zinazo 88 sawa na asilimia 7.6, Asia na Pacific 277 sawa na asilimia 24.0, Europe na north America 545 sawa na asilimia 47.2, pamoja na Latin America na Caribbean146 sawa na asilimia 12.7 jumla dunia nzima zikiwa ni 1154 huku maeneo mengine katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania yakisubiri kuingia katika orodha hiyo

About the author

mzalendoeditor