Featured Kitaifa

DK.CHAULA:’WADAU WA MAENDELEO TUENDELEE KUSHIRIKI KUPINGA VITENDO VYA UKATILI NCHINI’

Written by mzalendoeditor
KATIBU  Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Zainab Chaula, akizungumza na wadau wakati akifungua   Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Sekretariati ya Taifa ya kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto  kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalum,Sayi Magessa,akitoa maelezo kuhusu kikao hicho wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
Mratibu wa Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto,kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Bw.
Joel Mangi akiwasilisha hali ya Ukatili kwa sasa nchini wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Shirika la ICS Kudely Sokoine ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
 
MWENYEKITI wa Baraza la Watoto Taifa Nancy Kasembo,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
Meneja Miradi kutoka Shirika la ICS Bi.Sabrina Majitka,akitoa maelezo ya shirika hilo jinsi wanavyofanyakazi katika kutokomeza ukatili wa Wanawake na Watoto wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
Meneja Miradi kutoka Ubalozi wa Ireland Oliva Kinabo,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
AFISA Miradi kutoka Shirika la Women Fund Tanzania Trust Glory Mbia,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
AFISA Tathmini na ufuatiliaji kutoka Shirika ka Wildaf Fransisca Silayo,akizungumza wakati wa Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Wadau wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati akifungua   Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
KATIBU  Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum,Dkt Zainab Chaula, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa Tafakuri ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa Ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma.
………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum Dkt Zainab Chaula,amesema ni jukumu la wadau  wa Maendeleo nchini kushiriki Kikamilifu katika kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Dk.Chaula ameyasema hayo leo Desemba 13,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Tafakuri  ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.
Amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano (2017/18 – 2021/22), Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali zinazolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia maeneo nane (8) ya utekelezaji.
 “Kuna mafanikio yamepatikana kwenye utekelezaji wa mpango, hata hivyo ni muhimu kujiuliza kwanini vitendo vya ukatili bado vinaendelea kutokea licha ya jitihada mbalimbali za serikali na wadau.”amesema Dk.Chaula
Aidha Dk.Chaula amewataka  wadau kujipanga kutoa maoni ambayo yatasaidia kwenye mpango ujao ili kutokomeza vitendo hivyo.
”Mkutano huu utatuwezesha kubaini changamoto za kiutendaji zilizokwamisha jitihada mbalimbali katika kufikia malengo ya utekelezaji wa MTAKUWWA kuanzia ngazi ya Mtaa/Kijiji, Kata, Halmashauri, Mkoa na Taifa.”amesema 
Hata hivyo amesema kuwa Serikali imeendelea kuhakikisha ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto unatokomezwa nchini kwa kuendelea kuratibu Mipango  na Mikakati  inayosaidia katika kupinga ukatili wa aina zote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ICS Bw.Kudely Sokoine,amesema kuwa wataendelea kushikiana na Serikali kuhakikisha ukatili unatokomezwa kabisa nchini.
“Tumekuwa tukifanya utekelezaji katika maeneo sita ambapo tumekuwa tunatumia Mkakati  Jumuishi katika kuhakikisha tunatekeleza mpango kazi huu ambapo tunashirikisha wazazi,walezi,Walimu na Watoto na hata Mwenyekiti wa Baraza la watoto ni matokeo ya mkakati huo”amesema Bw.Sokoine.
Naye Meneja Miradi wa ubalozi wa Ireland, Oliva Kinabo, amesema kuwa  suala la kutokomeza mimba za utotoni linapaswa kubadilishiwa umri wa mtoto kutokana na sheria ya sasa kutamka umri wa kuolewa ni miaka 14 hadi 18.
Kwa upande wake  Afisa Miradi kutoka Shirika la Women Fund Tanzania Bi. Glory  Mbia amesema kuwa  Shirika  linafadhili vikundi mbalimbali vinavojikita katika kufikia wanawake na watoto kwa miaka Kumi nchini
“Tumekuwa tukitoa Ruzuku ,Ujenzi wa nguvu za pamoja kwani tunaamini katika ushirikiano na Mbinu hizi mbili zinalenga katika kuhakikisha wanawake na Wasichana wanafikiwa “amesema
Mwakilishi wa WILDAF ,Fransisca Silayo amesema Wataendelea kufanya kazi bega kwa bega na Serikali katika kuhakisha wanatokomeza ukatili wa watoto na wanawake na kusimamia eneo la kuhamasisha na kutoa elimu ili kuondokana na mambo ya mila na Desturi zisizofaa

About the author

mzalendoeditor