Featured Michezo

IHEFU FC YATIBUA UNBEATEN YA YANGA SC

Written by mzalendoeditor

HATIMAE Timu ya Ihefu imevunja rekodi ya Yanga ya kutokufungwa katika mechi ya 50 kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara baada ya kufungwa kwa mabao 2-1, mchezo ambao ulipigwa Mbarali mkoani Mbeya.

Yanga Sc ilianza kupata bao kupitia kwa Yannick Bangala kabla ya Never Tigere kusawazisha kwa kupiga mpira wa adhabu uliomshinda kipa wa Yanga na kutinga nyavuni moja kwa moja.

Bao la pili Ihefu Fc limefungwa na  Kissu  na kufanya matokeo kuwa 2-1.

Kwa Matokeo hayo Yanga wamebaki kileleni wakiwa na Pointi zao 32 wakiwa wamecheza mechi 13,Azam FC wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 32 wakiwa wamecheza mechi 14 huku Simba wakiwa wameshika nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 31 wakiwa wamecheza mechi 14.

About the author

mzalendoeditor