Featured Kitaifa

MABALOZI WARIDHISHWA NA MIPANGO YA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

Written by mzalendoeditor

Mabalozi wa Tanzania wameahidi kufanya kazi kwa karibu na Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma ili iweze kutekeleza mpango mkakati iliyojipangia wa kutoa huduma bora za afya nchini

.
Mabalozi walitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dkt. Alphonce Chandika kilichofanyika leo jijini Dar Es Salaam kujadili namna Mabalozi watakavyoweza kuvutia wadau watakaoshirikiana na hospitali hiyo kutekeleza mpango mkakati huo.
 
“Umeongea mengi na yote uliyoyaongea unaonekana unayaishi na umedhamiria yatokee, ni jambo jema kuwa na dira inayoonesha hospitali inapoelekea katika kuimarisha huduma za afya nchini”, Mwakilushi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Balozi Maimuna Tarishi alisema.  
 
Dkt. Chitanda aliwaeleza Mabalozi hao mipango ya hospitali hiyo ya kuanzisha huduma mbalimbali za kibingwa na kuimarisha zilizopo, hivyo aliwomba mabalozi kutafuta wadau kwenye maeneo yao ya uwakilishi ili washirikiane na hospitali hiyo kuimarisha huduma za afya nchini.
 
Baadhi ya maeneo ambayo Mkurugenzi aliomba Mabalozi washirikiane ni pamoja na huduma za matibabu ya magonjwa ya mfumo wa mkojo, saratani, moyo, upandikizaji wa figo na uboho na upasuaji wa nyonga na mishipa ya fahamu. Misaada inayohitajika ni pamoja na mafunzo ya kibingwa, ujenzi wa majengo na ununuzi wa vifaa tiba. 
 
Mabalozi wa Tanzania walikuja nchini kushiriki Mkutano na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba 2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akiongea na Mabalozi wa Tanzania kuhusu mipango ya hospitali hiyo yenye lengo la kutoa huduma bora kwa jamii. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti, Dkt. Monica Kessy.

 

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Amidi wa Mabalozi, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati), Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Genrva, Balozi Maimuna Tarishi (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afruka Mashariki, Bslozi Swahiba Mndeme wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

 

Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Ufaransa, Japan na Brazil wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

 

Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Urusi na Austria wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

 

Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania wakiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania

 

 

About the author

mzalendoeditor