Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi , wahadhiri pamoja na wahitimu mbalimbali wakati wa Mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, Mahafali yaliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiongozana na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine wa chuo hicho wakati aliposhiriki Mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, Mahafali yaliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiongoza viongozi , wahadhiri pamoja na wahitimu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania katika kuimba Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, Mahafali yaliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akishiriki Mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, Mahafali yaliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza leo tarehe 24 Novemba 2022.( Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi , wahadhiri pamoja na wahitimu mbalimbali wakati wa Mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, Mahafali yaliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiagana na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda mara baada ya kushiriki Mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania, Mahafali yaliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza
………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa vyuo vyote hapa nchini kuhakikisha elimu inayotolewa inaendana na mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea kwa kasi duniani na vipaumbele vyetu vya kitaifa ikiwamo ujenzi wa uchumi wa viwanda na uchumi wa buluu.
Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 24 Novemba 2022 akiwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 41 ya Chuo Huria Tanzania yaliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Amesema ni lazima kujipanga kutoa elimu iliyo bora na hasa inayolenga kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiajiri na zaidi na kuwa na ubunifu ambao utawasaidia kushiriki katika fursa zinazojitokeza na kujenga mihimili ya Taifa kiuchumi na kiteknolojia.
Makamu wa Rais amesema ili Tanzania iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati inayoongozwa na viwanda ni lazima kuwa na mifumo bora ya elimu hususan elimu ya juu.
”Serikali imeendelea kuwekeza katika sekta ya elimu ya juu na ufundi stadi kwa kuimarisha miundombinu, kuongeza bajeti kwenye sekta hiyo kila mwaka na kuendelea kuboresha sera ya elimu hapa nchini.”amesema
Pia ametoa rai kwa wanazuoni wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na vyuo vingine vyote hapa nchini, kutumia weledi na utaalamu wao katika zoezi la maboresho ya elimu.
Pia amewasihi wahitimu wa Chuo hicho kudhihirisha elimu waliopata katika utendaji wa kazi na maisha ya kila siku, iwe ni katika sekta rasmi au sekta isiyokuwa rasmi.
Amesema ni Lazima kuonesha utofauti katika kutafuta majibu ya maswali mbalimbali yanayowakabili Watanzania katika jitihada zao za kujiletea maendeleo.
Makamu wa Rais amesema kwamba Serikali imejipanga kuona sekta ya elimu inaboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji na kuweza kuendana na jitihada za kuleta maendeleo endelevu nchini ikiwemo kuendelea kuboresha mazingira ya Vyuo na kuongeza idadi katika mikoa yetu yote ili wananchi zaidi wapate fursa ya kujiendeleza kimasomo na kupata elimu ya juu.
Kwa kuzingatia kuwa utoaji wa elimu huria na masafa unategemea mifumo bora ya TEHAMA, Makamu wa Rais amesema Serikali ina mpango wa kuhakikisha Vyuo vyote vya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania vinaunganishwa kwenye mkongo wa Mawasiliano wa Taifa.