Featured Michezo

YANGA YAISHUSHA AZAM FC,SIMBA SC,MAYELE HAKAMATIKI

Written by mzalendoeditor

MABINGWA Watetezi Yanga amefikisha ”Ubeaten”48 sawa na dakika 4,320 tangu ilipofungwa mara ya mwisho na Azam FC April 25,2021  baada ya kuichapa Mabao 2-0 Dodoma jiji Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Liti mjini Singida.

Akiwa kwenye fomu ya kucheka na nyavu Mshambuliaji hatari kwa sasa ndani ya Lingi Kuu Fiston Mayele aliwanyanyua mashabiki wa Yanga dakika ya 42 akifunga bao la uongozi akimalizia pasi ya Tuisila Kisinda.

Kipindi cha Pili kilianza kwa timu zote kucheza mchezo wa kushambuliana na mnamo dakika ya 67 Fiston Mayele alirudi tena kambani akifunga bao la pili akimalizia pasi ya Denis Nkane na Sasa Fiston Mayele amefikisha mabao 8 na kuongoza katika chati ya ufungaji wa Ligi.

Kwa ushindi huo Yanga wamerejea kileleni kwa kufikisha Pointi 29 wakiwa wamecheza mechi 11 na kuishusha Azam FC yenye Pointi 29 huku ikiwa imecheza Mechi 13,Simba wameshuka nafasi ya tatu wakiwa na Pointi 27 wakiwa wamecheza Mechi 12.

About the author

mzalendoeditor