Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR AZITAKA TAASISI ZA SMZ KUSIMIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA

Written by mzalendoeditor

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezitaka Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusimamia Matumizi ya Fedha za Serikali ili kurejesha heshima ya Fedha Nchini.

Mhe. Hemed ameeleza hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Idara ya Uratibu za Shughuli za SMZ Dodoma alipokutana nao Afisini kwake Dodoma.

Ameeleza kuwa Taasisi nyingi za Serikali baadhi ya huduma husita kwa kisingizio cha ukosefu wa Fedha ambapo baadhi ya maeneo huhitaji Busara na Maamuzi sahihi katika Matumizi.

Aidha Mhe. Hemed ameeleza kufurahishwa kwake kuona Watendaji wa Idara hiyo wanawajibika ipasavyo licha ya changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo.

Amefafanua kuwa ni dhahiri Juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni zinaonekanwa na wengi ambapo ameahidi kuwa Ofisi kuwa ya mwanzo kuunga Mkono Juhudi hizo.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Idara hiyo kwa kuendeleza mashirikiano baina yake na Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hatua ambayo itawarahisishia Maraisi wote wawili kuweza kutumiza malengo yao ya kuwatumikia Wananchi wao.

Kuhusu uendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Tawi la Dodoma Mhe. Hemed amefurahishwa na hatua ya Benki hiyo kufungua Tawi Jijini Dodoma eneo ambalo ndio Makao Makuu ya Tanzania ambalo linawahitaji wengi wa Benki hiyo.

Amesema Benki hiyo imeonesha utayari wa uwajibikaji kwa kuanza vyema Biashara na kuwataka kuingia katika ushindani wa kibiashara wa ubora wa Huduma wakizingatia PBZ ni Benki Kongwe Nchini.

Nae Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dkt. Islam Seif Salum amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Wizara itasimamia Changamoto zote zinazoikabili Idara hiyo ikiwemo Ukosefu wa Magari upungufu wa Wafanyabiashara na Changamoto nyengine.

Aidha ameutaka Uongozi wa Idara hiyo kuwasilisha Taarifa ya Mapendekezo ya Utatuzi wa Changamoto ambapo amewataka kuzingatia Mfumo wa Mtandao (E Office) katika kuandaa Miundombinu ya Ofisi.

About the author

mzalendoeditor