Featured Kitaifa

WAJUMBE WATAKIWA KUFANYA UAMUZI WA BUSARA KUCHAGUA VIONGOZI.

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna-DODOMA

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), Gilbert Kalima,amewataka wajumbe kuchagua viongozi watakaotengeneza timu itakayoleta maendeleo na kukifanya chama kuzidi kuwa imara.

Hayo ameyasema leo Novemba 18,2022 jijini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma ambapo amewataka kutumia busara kuchagua viongozi watakaosimamia umoja ndani ya Chama kwa kipindi cha miaka mitano.

Bw.Kalima amesema kuwa  uchaguzi huo ni wa kutengeneza safu ya kukipatia ushindi chama hicho katika chaguzi mbalimbali ikiwamo uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

”Mnapochagua viongozi kumbukeni kuwa tunaanda  safu ya ushindi wa CCM mwaka 2025,ya kuipatia  CCM mwaka 2025, na ushindi wa CCM katika chaguzi zozote zitakazofanyika,”amesema Bw.Kalima

Ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo jumuiya hiyo iweke mikakati ya kujiimarisha kiuchumi.

“Mjielekeze katika kuweka mipango na mikakati ya kuhakikisha jumuiya yetu inaondoka hapa ilipo na kujiimarisha kiuchumi kadri inavyowezekana,”almesema

Hata hivyo amesema kuwa miaka mitano ijayo wahakikishe chama kinakuwa imara zaidi kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

Kwa upande wake,Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, amesema kuwa wasimamizi wa uchaguzi wanatekeleza wajibu wao wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika salama.

Awali Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Dk.Damas Mukasa, amesema kama Jumuiya katika kipindi cha miaka mitano wameweza kuimarisha umoja pamoja na kusimamia sera ya Jumuiya na uchumi

About the author

mzalendoeditor