Featured Kitaifa

MAMLAKA ZA MAJI NCHINI ZATAKIWA KUTOA TAARIFA SAHIHI ZA HUDUMA YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

Written by mzalendoeditor

MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

 

SEHEMU ya Watendaji kutoka Mamlaka za Maji wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,(hayupo pichani)  wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (katikati) akifatilia mada mbalimbali wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.Kulia ni Mhandisi Adam Ishara kutoka Wizara ya Maji na kushoto Meneja Ufundi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA Mhandisi Titus Safari.

MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mamlaka za maji na Miradi ya kitaifa mara baada ya kufungua kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa Mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22 kilichofanyika leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma.

……………………………………..

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi  Modestus Lumato, amezitaka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini kuhakikisha zinatoa taarifa sahihi za huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wananchi ili kushamirisha upatikanaji wa huduma endelevu kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Lumato ametoa maelekezo hayo leo Novemba 14,2022 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha Watendaji wa Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya Kitaifa kilicholenga kuhakiki taarifa za utendaji wa mamlaka hizo kwa mwaka 2021/22.

Mhandisi Lumato ameeleza kuwa tathmini iliyofanywa na EWURA imebaini kuwapo mamlaka za maji ambazo zimeendelea kuwasilisha taarifa zenye mapungufu kwenye kukidhi viwango vya huduma, uchakavu, ufanisi wa makusanyo wa maduhuli, muda wa upatikanaji wa huduma, ubora wa maji pamoja na idadi ya wananchi wanaopata huduma, hali hii inakwamisha kufanya tathmini ya hali halisi ya utendaji na upatikanaji huduma.

“Nitoe wito kwa mamlaka zote za maji kuhakikisha zinafanya masahihisho kwenye taarifa zenye mapungufu ili ziweze kutoa hali halisi ambayo mwisho wa siku itasaidia katika kupima utendaji na ufanisi wa huduma wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira” amefafanua  Mhandisi Lumato

Kwa upande wake Mwakilishi wa katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Adam Ishara,amezitaka Mamlaka hizo kujitahidi kutekeleza wajibu wake kwa kutoa takwimu sahihi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa huku akisisitiza kuwa, Wizara ipo tayari kutoa miongozo na ushirikiano unaohitajika muda wowote.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira,ambaye ni Meneja Ufundi wa Maji na Usafi wa Mazingaira EWURA, Mhandisi Titus Safari,amesema kuwa mchakato wa maandalizi ya ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji ni shirikishi hivyo kila mamlaka itumie kikao hicho kuthibitisha usahihi wa taarifa zake.

WATENDAJI  kutoka Mamlaka 25 za Majisafi na Usafi wa Mazingira za miji mikuu ya mikoa na mamlaka 7 za miradi ya kitaifa wamehudhuria kikao kazi hicho kinachofanyika makao makuu ya EWURA jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor