Na Bolgas Odilo-MZALENDO BLOG
AKIANZA kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza Kijana Clement Mziza ameing’arisha Yanga ugenini baada ya kuichapa bao 1-0 timu ya Kagera Sugar mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Yanga ilipata bao dakika ya 18 Clement Mziza aliwanyanyua mashabiki wake licha ya Mvua kunyesha katika jiji la Mwanza akimalizia pasi ya Fei Toto.
Mnamo dakika ya 70 Kagera Sugar walipata Penalti baada ya golikipa wa Yanga kumchezea rafu Hamiss Kiiza hata hivyo Erick Mwijage alikosa Penalti iliyopanguliwa na Djugui Diarra.
Kwa ushindi huo Yanga wamerejea Kileleni kwa kufikisha Pointi 23 huku wakiwa wamecheza mechi 9,Azam FC wameshuka nafasi ya pili kwa pointi 23 wakiwa wamecheza mechi 11,Simba wakibaki nafasi ya tatu kwa Pointi 21.