Featured Michezo

SINGIDA BIG STAR YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI DHIDI YA SIMBA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Singida Biga Star imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara iliyochezwa uwanja wa Liti Mjini Singida.

Singida Big Star walianza kupata bao kupitia kwa nyota wao Deus Kaseke akipokea krosi kutoka kwa Hamisi Ndamla katika dakika za mwazo kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba walisawazisha bao kupitia kwa Peter Banda hadi mwamuzi anapuliza kipyenga cha Mwisho timu hizo zimeweza kugawana Pointi.

Kwa Matokeo hayo Simba wamebaki nafasi ya pili wakiwa na Pointi 18 huku Singida wakibaki nafasi ya nne wakiwa na pointi 18

About the author

mzalendoeditor