Featured Kitaifa

DC MBONEKO ARIDHISHWA KAZI YA UJENZI VYUMBA MADARASA SHY DC NA MANISPAA YA SHINYANGA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akifyatua matofali katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akishiriki kujenga vyumba vya madarasa katika Shule mpya ya Sekondari Salawe katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Shinyanga ili kuona utekelezaji wa miradi hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo leo Novemba 9, 2022 , Mboneko amesema
 amefanya ziara hiyo kuona hatua ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa, ili vikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa kwa kuendana na thamani halisi ya fedha (value for money), na mwaka 2023 vianze kutumika kufundishia wanafunzi.

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika halmashauri zetu hizi mbili (Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Shinyanga) ametoa kiasi cha fedha Sh. bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 109, Manispaa ya Shinyanga vyumba 61wilaya ya Shinyanga vyumba 45, na kasi yake ya ujenzi ni nzuri na wanafunzi watayatumia mwaka 2022,” amesema Mboneko.

Aidha, amesema wanafunzi wote ambao watachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wote wahudhuria shule na hakuna hata mmoja kukosa, ikiwa elimu ni bure na wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao.

Nao baadhi ya madiwani akiwemo Mussa Andrew wa Kolandoto na Awadhi Mbaraka wa Solwa, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha na kufanikisha ujenzi huo wa vyumba vya madarasa ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani ili wasome katika mazingira Rafiki.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Deus Maganga, amesema madarasa Saba ambayo wamepewa na Rais Samia shuleni hapo yamemaliza kabisa upungufu uliopo na wanafunzi watasoma bila ya kubanana.

Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Josephine Juma kutoka Kolandoto Sekondari, wamesema wanaposoma kwa kujinafasi hata masomo wanaelewa vizuri, kuliko kusoma kwa kubanana ambapo inakuwa vigumu kuelewa masomo na hatimaye kufanya vibaya kutaaluma.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumzia ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani.

Diwani wa Solwa Awadhi Mbaraka akitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa, pamoja na usimamizi mzuri wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kuhakikisha madarasa hayo yana kamilika kwa wakati.

Mkuu wa shule ya Sekondari Kolandoto Deus Maganga akielezea namna vyumba 7 vya madarasa shuleni hapo vitakavyo maliza upungufu na wanafunzi kusoma kwa nafasi.

Mwanafunzi Patric Shija wa shule ya Sekondari Kolandoto akielezea umuhimu wa vyumba vipya vya madarasa shuleni hapo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akishiriki kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga kwa kufyatua matofali.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea kufyatua matofali katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Diwani wa Solwa Awadhi Mbaraka akishiriki na yeye kufyatua matofali katika shule mpya ya Sekondari Solwa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Salawe.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ubora wa matofari.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ubora wa matofari.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Kolandoto ukiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Muonekano wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa ukiendelea.

ujenzi wa darasa katika shule ya Sekondari Ghembe wilayani Shinyanga ukiendelea.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iselamagazi wilayani Shinyanga ukiendelea.

About the author

mzalendoeditor