Featured Kitaifa

KANZIDATA YA KUWATAMBUA WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA YAANZISHWA

Written by mzalendoeditor
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)Bi. Beng’i Issa ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 8,2022 Jijini Dodoma kuhusu dhumuni la kuanzishwa kwa Kanzidata ya taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) imeanzisha kanzidata ya kuwakutanisha na kuwaunganisha wawekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi wa kampuni za nje na wafanyabishara wadogo na wakubwa wa ndani ya nchi.
Hayo yamesemwa leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Beng’i Issa,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa Wafanyabiashara,Wawekezaji, watoa huduma ,mifuko ya Uwezeshaji na vikundi mbalimbali kujiunga na Kanzidata ya taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Bi. Beng’i amesema kuwa kwa kutumia kanzidata hiyo itaziba pengo la kutokujuana na kutojua wafanyabiashara wapi wanafanya biashara gani na wanahitaji nini na wako wapi hapa nchini.
“Lengo kuu ni kuwaunganisha Wawekezaji na wafanyabiashara huku utafiti ukionesha kuwa kuna pengo kati ya makundi haya mawili, niseme tu hili ni jukwaa tosha la kuwakutanisha haya makundi na Asasi za kifedha ,mifuko ya uwezeshaji na vikundi vya kifedha vya kijamii hivyo naamini watakopesheka,”
Na kuongeza kuwa “Pengo la kwanza ni kutojulikana nani ana nini na nani anahitaji nini na yuko wapi,” amesema Bi. Beng’i 
Bi. Beng’i amesema kuwa utafiti unaonesha kwamba kuna pengo kati ya makundi haya mawili. Pengo hilo pia ni  kitojuana nani ana nini na anahitaji nini na yupo wapi.
“Kanzidata hiyo ya Taifa ya Uwezeshaji imeanzishwa kuziba hili pengo, ni fursa kwa Watanzania hasa wafanyabishara wakubwa na wadogo wajitokeze kujiunga na chombo hiki ili wawekezaji wajue nani ana nini,” amesema Bi. Beng’i 
Aidha ameongeza kuwa Kanzidata hiyo itaisaidia Serikali kuratibu manunuzi ya ndani na kutoa fursa kwa makampuni zinazowekeza kufahamu bidhaa zinazopatikana kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani.
Amesema kuwa katika Kanzidata pia baadhi ya wafanyabiashara hususani wadogo ambao hawana mitaji ya uhakika,hivyo itakuwa ni jukwaa la kuwafikia mifuko ya uwezeshaji ambayo inatoa mitaji kwa riba ndogo na masharti nafuu.
“Kanzidata hii haikuwasahau Mama lishe na Baba lishe ,Vikundi mbalimbali vya vijana ambao wanafanya shughuli ndogondogo za kiuchumi tunawashauri wajiunge kwenye vikundi vya pamoja za kiuchumi,kama wauzaji wa bidhaa za vyakula, wachomaji gril,watengeneza Samani mbalimbali za nyumbani na wenye ujuzi wowote ule wajisajili na hatimaye wajiunge na Kanzidata hii ili Watambulike,”amefafanua  Beng’i
Kwa upande wake Meneja wa Tehama na Takwimu wa Baraza hilo Isaac Dirangw ,amesmea kuwa Kanzidata hiyo inalenga kuwatambua wafanyabishara wengi ambao wanafanya biashara bila kutambulika.
”Mbali tu na bidhaa zako na huduma zako kwa ujumla kujulikana pia kuna fursa kubwa ya kupata mikataba na Makampuni makubwa na viwanda vikubwa , ikiwemo pia kujumuishwa katika mashindano makubwa ya kuwania tuzo katika Kongamano la kila Mwaka la Uwezeshaji Kiuchumi,”amesema Dirangw
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)Bi. Beng’i Issa ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Novemba 8,2022 Jijini Dodoma kuhusu dhumuni la kuanzishwa kwa Kanzidata ya taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
MENEJA wa Tehama na Takwimu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Isaac Dirangw,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 8,2022 Jijini Dodoma  kuhusu dhumuni la kuanzishwa kwa Kanzidata ya taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

About the author

mzalendoeditor