Featured Kitaifa

NDEGE YA PRECISION AIR YAANGUKA ZIWA VICTORIA

Written by mzalendoeditor
Ndege ya Shirika la Precision Air imepata ajali katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera.
Akizungumza kwa njia ya simu leo Jumapili 6, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha taarifa za ajali hiyo na kusema kuwa yupo kwenye eneo la tukio akiendelea na uokoaji.
“Iko sahihi hiyo taarifa niko kwenye eneo la tukio nafanya uokozio, siwezi kuzingumza zaidi” amejibu kwa kifupi Kamnda Mwampaghale alipopigiwa simu.
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha ndege hiyo ikiwa imetumbukia kwenye maji.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa ndege hiyo imepata ajali jirani na Uwanja wa Ndege wa Bukoba huku taarifa zingine zikidai kuwa abiria 23 wameokolewa kati ya 49 na uokoaji unaendelea.

About the author

mzalendoeditor