Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wananchi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato,leo Oktoba 30,2022 jijini Dodoma.
……………….
” Ndugu zangu najua kuna tabia za baadhi ya wale mnaopewa kazi za muda(vibarua) wakipewa kusimamia ujenzi wanakuwa na vijitabia vya kudokoa dokoa mara Mfuko wa misumari,mara saruji hii sio sawa nataka mtakaopata nafasi msijihusishe na vitendo hivo,”amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia amesema kuwa ujenzi huo lengo ni kukuza ushindani unakuwepo wa kimataifa na pia ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwani ndege za kimataifa zitakuwa zikiendesha safari zake na pia soko la bidhaa litaongezeka.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mnyaa Mbarawa amesema Mradi huo utakuwa na fursa kwa Wakazi wa Dodoma na Mikoa mingine pamoja na kuiunganisha nchi na Mataifa mengine na kuahidi kusimamia ili ujenzi huo umalizike kwa wakati.
”Nia ya kujenga uwanja ilikuwepo tangu mwaka 1970 ambapo kiwango cha Ujenzi ni daraja E kwa mujibu wa viwango vya kimataifa na wataanza na ujezni wa barabara ya ndege kupaa kilomita 3.6 na utakuwa na uwezo wa kuwahudumia abiria Milioni 1.5 kwa mwaka.”amesema Prof.Mbarawa
Naye Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema Bunge litaendelea kumuunga mkono Rais Samia na kusema NDIYO kwenye bajeti ya Serikali kwa miradi mikubwa ya kimkakati na miradi mipya ambayo Serikali imepanga kutekeleza.
” Tumesikia hapa kuwa safari yako ya Ufaransa imewezesha kufanyika matengenezi makubwa ya jengi la pili la abiria katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, hivyo Bunge litaendelea kusema NDIYO kwa safari zako za nje. Hivyo ni kuahidi, Bunge litaendelea kusema NDIYO kwenye miradi ya maendeleo, tutakosoa panapobidi na kutoa ushauri.”
Katibu wa NEC itikadi na ueneze Chama Cha Mapinduzi CCM Shaka hamdu Shaka,ameipongeza serikali kwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa vitendo na kuviasa vyama vingine vya siasa nchini kuunga mkono jitihada zinazofanywa za kuwaletea wananchi maendeleo.
“Rais Samia anaendeleza maono ya makao makuu ya nchi kuwa Dodoma hili halipingiki tunaona jinsi anavyoendelea kuipa heshima na thamani makao makuu ya nchi hivyo anaviasa vyama vingine vya siasa nchini kuunga mkono jitihada zinazofanywa za kuwaletea wananchi maendeleo.”amesema Shaka.
Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila, amesema kuwa eneo hilo lina ukubwa wa hekta 4500 na Sh.Bilioni 15.20 zimetumika kulipa fidia wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya mradi.
Mhandisi Mativila amesema kuwa mwaka 2015 serikali ilipata mkopo wa masharti nafuu kutoka AfDB kwa ajili ya marejeo ya upembuzi yakinifu na usanifu kwa kina ambapo mwaka 2017 serikali kupitia TAA iliingia mkataba na kampuni ya kihandisi ya nchini Tunisia kwa kampuni ya Tanzania kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 1.885 ambapo kazi hiyo ilikamilika mwaka 2019.
“Kiwanja hiki lengo kijengwe kiwe na uwezo wa kuhudumia abiria Milioni 32 kwa mwaka, kiwango ambacho kitafikiwa baada ya miaka 100,”
Naye , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema jumla ya wakazi wa Dodoma 3,368 wamelipwa fidia ya Sh bilioni 16.93 kupisha ujenzi huo ambapo wananchi 10 wanaodai fidia ya Sh milioni 80 wameshapelekwa maombi Hazina.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dk Patricia Laverley,amesema kuwa ujenzi wa kiwanja hicho umefadhiliwa na benki yake kwa gharama ya dola za Marekani milioni 271 ambao utachukua miaka mitatu.
“ Tunachotaka ni kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya Dodoma inavyotakiwa kuwa kwa kuimarisha usafiri anga kwa kuruhusu ndege za kimataifa kutua hapa nchini hatua ambayo itasaidia kuibadili Tanzania.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura ,amesema mpaka Machi 2021 Tanzania ilikuwa na viwanja vya ndege 435 ambapo Serikali inamiliki viwanja 194 na viwanja vya sekta binafsi ni 241 ambapo viwango vya kimataifa vya ulinzi na usalama ni asilimia 69 kwa mwaka 2022 na lengo ni kufikia asilimia 75 katika kaguzi za mwaka 2023/24.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wananchi kabla ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato,leo Oktoba 30,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makame Mnyaa Mbarawa,akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Oktoba 30,2022.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Rogatus Mativila, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Oktoba 30,2022.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dk Patricia Laverley,akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Oktoba 30,2022.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Msalato jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo Oktoba 30,2022.
Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato jijini Dodoma leo Oktoba 30,2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Meneja Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Patricia Leverley kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Mkoani Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali.