Na Bolgas Odilo,Mzalendo blog
HATIMAYE Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam kutoka Chamazi Timu ya Azam FC imefuta uteja wa kuendelea kufungwa na Simba baada ya kukaa miaka 6 bila kupata ushindi leo wamepata ushindi wa bao 1-0 mchezo uliopigwa uwanjwa wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Shujaa wa Azam FC ni Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe Prince Dube dakika ya 34 akiachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Simba Aisha Manula.
Kwa ushindi huo Azam FC wamefikisha Pointi 14 na kushika nafasi ya nne wakiwa wamecheza mechi nane huku Simba wakibaki nafasi ya tatu wakiwa wamecheza mechi 7 na Mabingwa watetezi Yanga wanaongoza msimamo wakiwa na Pointi 17 nafasi ya pili inashikwa na Mtibwa Sugar wakiwa na Pointi 15.