Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YAISHAURI TBA KUJENGA MAGHOROFA KATIKA MIRADI YAKE

Written by mzalendoeditor

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo , wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iliyofanyika leo Oktoba 25,2022 bungeni, jijini Dodoma.

………………………

Na Eva Godwin-DODOMA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka serikali kuiongezea uwezo wa rasiliamali watu na fedha Wakala wa Majengo nchini (TBA) ili kuimarisha utendaji kazi wao.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 25,2022 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati hiyo,Mhe.Selemani Kakoso,wakati wa kamati hiyo ikipokea taarifa ya utekelezaji wa TBA katika robo ya mwaka 2022/23.

Mhe.Kakoso ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha inawatafutia TBA watumishi wa kutosha kwa kuomba kibari cha kuajiri hasa kutokana na miradi inayotekelezwa na taasisi hiyo kuhitaji sana usimamizi wa karibu.

 “Nikuombea nendeni mkalisimea, tafuteni kibari ili muajiri watu watakojua kufanya kazi, kwasababu kazi za TBA zinahitaji sana usimamizi na mkifanya hivyo kutakuwa na mapinduzi makubwa sana kwenye sekta ya unjenzi.”amesema Mhe.Kakoso

Amesema kuwa  Wizara imekuwa ikiepelekewa fedha nyingi, ni vyema kuangalia namna ya kuitumia TBA ambayo ina fursa ya uwekezaji ili kuwekeza na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo, fedha nyingi zitarudi serikalini kupitia uwekezaji huo.

 “ Naamani wizara mnapata fedha nyingi, zingine zipitisheni TBA kwasababu wananafasi ya uwekezaji, kwa mipango na uwezo wa TBA wananafasi kubwa ya kufanya majenzi, mfano mkiwawezesha hata pale  Magomeni Kota wanaweza kujenga mall na kuibadilisha mabadiliko makubwa sana kwenye jiji la Dar es Salaama na kuwa na uwekezaji mkubwa atakaoleta faida kwa serikali.”

 Aidha amesema wakati wa maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24, Wizara ihakikishe inaitegea TBA bajeti ya kutosha ili kuweza kutekeleza miradi mingi ambayo italeta tija kwa serikali.

 “ Mkianza maandalizi ya kuandaa bajeti ya wizara hakikisheni TBA inatengewa bajeti ya kutosha, maana TBA wenyewe wamesema wakipewa shilingi bilioni 50 ambazo kwa serikali ni fedha kidogo na sitafanya wafanye majenzi makubwa ambayo watu wataweza kukodi na kuishi na pia fedha hizo zitarudi ndani ya serikali.”

Hata hivyo ameitaka TBA kuhakikisha inajenga maghorofa kwenye miradi ya nyumba za makazi wanazojenga.

“ Tumeipokea taarifa ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na tunawapongeza kwa kazi kubwa mnayoifanya katika kutekeleza kazi ya majenzi ya nyumba, sasa tuwashuri badala ya kuendelea kujenga nyumba za chini, jengeni maghorofa kama ilivyofanya pale Magomeni Kota.”

Naye Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch.Daud Kondoro amesema kuwa  watakwenda  kutekeleza maagizo ya kamati na kusisitiza kuwa Wakala umejipanga kuhakikisha inatekeleza miradi yake kwa kasi, ubora na haraka.

“ Wakala tumejipanga kuhakikisha miradi yetu yote tunayotekeleza tunaitekeleza kwa kasi, haraka ikiwa ni ubora.”

Kondoro amesema katika robo ya kwanza ya mwaka 2022/23, Wizara imeipatia TBA  zaidi ya Sh bilioni 8 kwa ajili ya kuendelea kutekeleza miradi yake.

“ Tunaishukuru Wizara katika robo ya mwaka tumepewa shilingi bilioni nane kwa ajili ya kutekeleza miradi yentu nah ii ni sawa na moja ya tatu ya ya fedha ztulisokuwa tumetengewa kwa ajili ya utekelezaji miradi.”

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo , wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iliyofanyika leo Oktoba 25,2022 bungeni, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) iliyofanyika leo Oktoba 25,2022 bungeni  jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Tanga, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Mwanaisha Ulenge, akichangia hoja  wakati wa kamati hiyo kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TBA iliyofanyika leo Oktoba 25,2022 bungeni jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakifuatilia taarifa ya Utendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania  (TBA) ilipowasilishwa kwa  kamati hiyo,leo Oktoba 25,2022 bungeni jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor