Featured Kitaifa

WAZIRI JAFO ATAKA UPANDAJI MITI UWE ENDELEVU KUPAMBANA NA MABADILIKO TABIANCHI,AIPONGEZA BENKI YA STANDARD CHARTERED KUPANDA MITI ELFU MOJA.

Written by mzalendoeditor

Waziri
wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Seleman Jaffo
(katikati), akipanda mmoja ya miti 1000 iliyotolewa na Benki ya Standard
Chartered iliyopandwa katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo
Mkoa wa Pwani na (kushoto) ni Afisa Tawala wa Wilaya Magamoyo, Casilda Mgeni, na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende.

…………………………..

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemani
Jafo amesema ni vema suala la upandaji miti katika nchi yetu liwe
endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira.

Jafo aliyasema hayo
leo Oktoba 23,2022 baada ya kuongoza upandaji miti uliofanyika katika
Shule ya Msingi Mtoni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kuratibiwa na
benki ya Standard Chartered ambapo amewahimiza wananchi kuendelea
kuhamasisha kupanda miti.

“Upandaji wa miti kwa wingi kwenye
mazingira ni njia mojawapo itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya
hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya mwanadam”,alisema Japo.

Jafo
ameipongeza Benki ya Standard Chartered kwa kumualika katika zoezi la
upandaji miti katika shule hiyo na kwamba ameomba taasisi za Serikali na
binafsi nchini kuiga mfano wa Benki ya Standard Chartered kwa hatua ya
kuleta miche ya miti 1000

Amesema ajenda ya mazingira ndiyo
ajenda inayosababisha uchumi kuwa imara,lakini pia akawataka wanafunzi
kupeleka ujumbe kwa wazazi wao kushiriki zoezi zima la kupanda Miti
katika maeneo yao.

“Serikali imekuwa na mikakati mbalimbali
katika kuhakikisha inatunza mazingira ili kuwa na mazingira safi,na
miongoni mwa mikakati hiyo ni upandaji miti katika taasisi za serikali
na binafsi nchini,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende amesema amefarijika
sana kuona watanzania wanapanda miti kwa wingi.

“Benki yetu
ya Standard Chartered itaendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali za
upandaji miti na kuhakikisha Tanzania inakua ya kijani kama maelekezo
ya Serikari ya kupanda miti katika maeneo yote nchi nzima,

Kwa
hiyo na sisi pamoja na Waziri Jafo tunashiriki kupanda Miti Elfu moja
(1000) katika shule hii katika hatua ya kupambana na mabadiliko tabianchi na kutunza Mazingira”,alisema


Waziri
wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Seleman Jaffo
(katikati), akipanda mmoja ya miti 1000 iliyotolewa na Benki ya Standard
Chartered iliyopandwa katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo
Mkoa wa Pwani na (kushoto) ni Afisa Tawala wa Wilaya Magamoyo, Casilda Mgeni, na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende akipanda mti
huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Dkt.Selemani Jafo akishuhidia katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana tarehe 22 Oktoba 2022.iliyotolewa na benki
ya Standard Chartered.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemani
Jafo akishuhudia Viongozi wa CCM Wilaya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakipanda
mti kwenye shule hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
Dkt. Selemani Jafo akikabidhiwa fulana kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende kushoto ni Afisa
Tawala Wilaya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Casilda Mgeni.


Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani
Jafo,akihutubia wadau mbalimbali wa Mazingira wakati wa upandaji miti
Elfu moja (1000) iliyotolewa na Benki ya Standard Chartered na kupanda
katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende akisoma
hotuba yake wakati wa upandaji miti Elfu moja (1000) iliyotolewa na
Benki hiyo iliyopandwa leo Oktoba 23,2022 katika Shule ya Msingi Mtoni
Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. (PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA WA
MICHUZI TV)


Wadau
mabalimbali wa Mazingira wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (hayupo
pichani)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 22 Oktoba 2022.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM Wilaya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana tarehe 22 Oktoba 2022.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Shule ya Msingi
Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Sehemu ya Mti .(PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)

About the author

mzalendoeditor