Featured Kitaifa

RAIS SAMIA KUZINDUA MATOKEO YA MWANZO YA SENSA 2022

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 21,2022   kuhusu uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kutangazwa Oktoba 31,mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

…………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua matokeo ya mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi Oktoba 31, mwaka huu katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.

Hayo yamesema leo Oktoba 21,2022 jijini Dodoma na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, wakatiakitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi huo ambapo amesema kuwa  shughuli hiyo itahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kiserikali pamoja na wawakilishi wa nchi mbalimbali ambao ni mabalozi watakaowakilisha nchi zao

RC Senyamule amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu tarehe 5 Septemba, 2022 wataalamu wetu walianza zoezi hilo la uchakataji wa taarifa. Hadi sasa matokeo ya mwanzo yako tayari kwa uzinduzi.
“Ninayo furaha kutangaza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan atazindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 tarehe 31 Oktoba, 2022 katika uwanja wa michezo wa Jamhuri jijini Dodoma,”amesema Senyamule
Aidha ametolea mifano Sensa zilizopita ikiwemo ile ya mwaka 2002na 2012 ambazo zilitumia teknolojia ya usomaji wa vivuli (Scanning Technology), matokeo ya Sensa hizo yalizinduliwa rasmi miezi mitatu baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu ,wakati Sensa ya mwaka 2022 matokeo yake yanazinduliwa mwezi mmoja baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu na makazi.
“Kwa Sensa ya mwaka huu, matokeo yake kama mnavyoona yatatoka ndani ya kipindi cha mwezi mmoja baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu watu ,ambapo ni mafanikio makubwa katika utekelezaji wa Sensa nchini kwetu na yamewezekana kutokana na matumizi makubwa ya tekinolojia za kisasa hasa matumizi ya vishikwambi katika awamu zote za utekelezaji wake na utashi wa Siasa katika kusimamia zoezi hilo kuanzia maandalizi hadi leo,” Amesema Senyamule
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wote Mkoa wa Dodoma, Taasisi zote, Watumishi wa Umma wote na wa Sekta binafsi Mkoani Dodoma, Makundi mbalimbali katika jamii (wafanya biashara, Dini, Walemavu, Bodaboda, Machinga, Wazee ) pamoja na wananchi kutoka Mikoa yote jirani kumuenzi Rais kwa kujitokeza kwa wingi tarehe 31 Oktoba, 2022 kwenye viwanja vya Jamhuri kujumuika katika katika tukio hilo.
Ikumbukwe kuwa Sensa ya watu na Makazi ilianza rasmi Agosti 23 Mwaka huu na kumalizika Septemba 5 Mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor