Featured Kitaifa

TANZANITE SUPPORT ORGANIZATION (TSO) YAENDELEA KUTOA ELIMU NA MAFUNZO MBALIMBALI KWA VIJANA

Written by mzalendoeditor


Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Mind Garden akiwafundisha vijana Elimu kuhusu Afya ya akili. Mind Garden wanatoa huduma mbalimbali katika masuala ya kitabia, kihisia, kisaikolojia na akili kwa watu wote wakiwemo watoto, vijana na watu wazima.

Vijana kutoka TSO – Tanzanite Support Organization wakiwa pamoja na Dr. Sylvia akiwafundisha Elimu ya Afya ya Uzazi na Hedhi salama. Faida za kupata elimu ya afya ya uzazi ni pamoja na: -Kuepuka mimba za utotoni -Kuepuka changamoto za uzazi -Kuepuka ndoa za utotoni na pia kuepuka kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa, etc

Bw. Rahim kutoka UTT Amis akitoa Elimu ya maswala ya Fedha na Uchumi kwa vijana wanaopatiwa mafunzo ya kujiendeleza katika shirika la Tanzanite support organization (TSO) Kampuni ya UTT AMIS inasimamia Mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu


Mazoezi ya viungo (YOGA)

Vijana wakifurahia jambo kwa pamoja wakati wakipata mafunzo

Bw. Beda Shayo kutoka kampuni ya Ahava Security Group (ASG) akizungumza na vijana na kuwapa mafunzo namna kampuni hiyo inavyofanya kazi. Baadhi ya vijana wameshaajiriwa katika kampuni hiyo ya Ahava security na wanaendelea na majukumu yao.

Vijana wakiwa Katika picha ya pamoja na bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Mind Garden

About the author

mzalendoeditor