Kaimu Mkurugenzi wa elimu ya juu kutoka wizara ya elimu Dkt. Evaristo Mtitu akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao kazi hicho mkoani Arusha.
…………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Bodi ya mikopo elimu ya juu (HELSLB) imewanao maofisa mikopo kutoka vyou vya kati na vya juu ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuhudumia dawati la wanafunzi ili kuweza kuboresha zaidi upatikanaji na utoaji wa mikopo hiyo.
Akifungua kikao kazi hicho Kaimu Mkurugenzi wa elimu ya juu kutoka wizara ya elimu Dkt. Evaristo Mtitu alisema kuwa uboreshaji wa huduma ya mkopo utasaidia kila mwanafunzi mwenye sifa kuweza kutimiza ndoto yake ya kupata elimu ya juu.
Dkt Mtitu alisema serikali wakati wote inaweka mikakati inayosaidia upatikanaji wa fedha za kutosha ili kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji na wanaotoka kwenye mazingira magumu ya kiuchumi waweze kupata elimu ya juu
Alieleza kuwa baada ya mafunzo hayo HESLB ni vyema wakahakikisha walengwa wanapata taarifa stahiki na maelekezo ili wanapoombwa kusiwepo kwa manung’uniko yoyote kwa wanafunzi wenye uhitaji wa mikopo
“Ni imani yangu wanafunzi wahitaji wa mikopo ya elimu ya juu watapata taarifa za kutosha na kwa wakati namna ya upatikanaji wa mikopo na mahitaji yanayotakiwa wakati wa kuomba mikopo,”amesema Dkt Mtitu.
Kwa wake mkurugenzi wa uchambuzi na upangaji wa mikopo kutoka HESLB Veronica Nyahende amesema kakao kazi hicho kitatoka na maazimio ya uboreshaji wa huduma ya hutoaji mikopo ili kuweza kuwafikia walengwa wanaoshindwa kutekeleza vigezo vya uombaji wa mikopo.
Naye Ofisa mikopo kutoka Chuo kikuu SUA,Santina Bugenyi amesema changamoto inayowakabili ni baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu kuhairisha masomo kutokana na kukosa fedha ya ada yote hivyo anaiomba bodi hiyo kuweka mazingira ya upatikanaji wa mikopo na utoaji wa taarifa kwa walengwa.
Hata hivyo Kamishna wa mikopo wa vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini,Emmanuel Martine anaishukuru serikali kwa kutenga kiasi cha sh.573 bilioniĀ kwa ajili ya elimu ya juu nchini na inakwenda kinufaisha zaidi ta vijana 640 hivyo ni matarajio yao huduma ya mikopo hiyo itaboreshwa na kuweza kuweka mikakati ya kudumu.
Kaimu Mkurugenzi wa elimu ya juu kutoka wizara ya elimu Dkt. Evaristo Mtitu akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua kikao kazi hicho mkoani Arusha.
Baadhi ya maofisa mikopo kutoka vyuo vya kati na juu wakiwa katika kiakao kazi na bodi ya mikopo elimu ya juu (HELSLB) mkono Arusha.