Na Alex Sonna,Dodoma
Dodoma Jiji imemtangaza kocha wa zamani wa Coastal Union,Melis Medo kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo.
Medo anachukua nafasi ya Masoud Djuma ambaye jana uongozi wa klabu hiyo ulimtupia virago na benchi zima la ufundi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 11 Jijini hapa ilieleza kuwa Dodoma Jiji wamefikia makubaliano na Medo kuwa Kocha Mkuu.
“Uongozi unawaomba mashabiki wetu na wapenda michezo kumpa ushirikiano wa kutosha kocha Medo katika kipindi chote atakachohudumu kama Mkuu wa benchi la ufundi,”ilieleza taarifa hiyo.