MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
……………………………..
Na.Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri amelipongeza shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Dodoma kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kuendelea kuboresha huduma kwa wateja.
Hayo ameyasema leo Oktoba 7, 2022 jijini Dodoma wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika hilo, ambapo amesema kuwa
“Niwapongeze kwa kuhitimisha wiki ya huduma kwa mteja, utoaji wa huduma ukiimarishwa hasa kwenye shirika hili muhimu, kutaleta tija kwa jamii, nawapongeza kwa kupiga hatua sana kwenye utendaji kazi wenu,”amesema Shekimweri
Aidha Shekimweri amesema kuwa kutokana na shirika hilo kupitia katika mifumo mipya ya kidijitali wanapaswa kwenda na kasi na viwango katika kutoa huduma iliyobora kwa wateja wao.
”Mnatakiwa kwenda sambamba na kasi ya ubunifu ili kuweza kutimiza malengo ya Serikali kwa wananchi na wadau wengine ambao ndio wateja wanaofikiwa na huduma hiyo.”amesema
Amewataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa ari, ushirikiano, ubunifu na kujituma kwa hali ya juu ili kuweza kutimiza malengo ya Serikali kwa wateja.
Aidha Shekimweri ameshiriki zoezi la kukata keki na watumishi wa TANESCO na wateja waliohudhuria hafla hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa TANESCO mkoa wa Dodoma, Mhandisi Donasiano Shamba, ametaja maboresho mbalimbali yaliyofanyika ndani ya miezi tisa iliyopita yanayolenga kutoa huduma bora kwa wateja wake.
Mhandisi Shamba amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza mpango mkakati wa miezi 18 wenye vipaumbele saba ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesema kupitia mfumo wa kidigitali wa kuomba kuunganishiwa umeme bila kumlazimu mteja kwenda ofisini (Nikonekt), shirika hilo limepokea maombi ya wateja zaidi ya 19,000 na tayari wananchi zaidi ya 10,000. wameunganishiwa umeme.
“Maboresho yamefanyika katika huduma za dawati la dharura ambapo wateja wanapiga simu kwenye kituo kikuu cha miito ya simu na wanapata huduma ndani ya muda mfupi zaidi” amesema Mhandisi Shamba.
Naye Mhandisi wa miradi na mitambo, kutoka kampuni ya Kilimo Pyxus, Muhoja Manane, amesema TANESCO imepiga hatua katika kuwahudumia wateja ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
Awali, Mwenyekiti wa wafanyakazi wa Shirika hilo kupitia Chama cha Wafanyakazi (TUICO), Ramadhan Butallah, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wateja wanapata huduma bora.
”Wateja wanapewa huduma kulingana na mwongozo wa mkataba wa huduma kwa mteja kwa kuhamasisha wafanyakazi kuwahudumia vyema wananchi.”amesema
TANESCO Mkoa wa Dodoma wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusheherekea wiki ya huduma kwa mteja inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba
MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akisisitiza jambo wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
Meneja wa TANESCO mkoa wa Dodoma, Mhandisi Donasiano Shamba,akitoa taarifa ya shirika hilo mkoa wa Dodoma wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
MENEJA Masoko wa TANESCO Bw.Kassim Chowo,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
Mhandisi wa miradi na mitambo, kutoka kampuni ya Kilimo Pyxus, Muhoja Manane,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa wafanyakazi wa Shirika hilo kupitia Chama cha Wafanyakazi (TUICO), Ramadhan Butallah,akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
BAADHI ya watumishi wa TANESCO wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri (hayupo pichani) wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Tanesco Mkoa Dodoma Sarah Libogoma,wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akikata keki wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akiwalisha keki wafanyakazi wa TANESCO,Wateja waliohudhuria kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma,Jabir Shekimweri,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuzungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.
WAFANYAKAZI wa TANESCO wakichangia damu wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja kwa Shirika la TANESCO Mkoa wa Dodoma hafla iliyoendana sambamba na ukataji wa keki pamoja na uchangiaji damu iliyofanyika leo Oktoba 7,2022 jijini Dodoma.