Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA AONGOZA HARAMBEE UNUNUZI KIWANJA CHA KANISA ROMBO//AWEZESHA KUPATIKANA SH.MILIONI 82.8

Written by mzalendoeditor

Na Mathias Canal, Rombo-Kilimanjaro

Mbunge wa Jimbo la Rombo Mkoani Kilimanjaro ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda leo tarehe 2 Octoba 2022 ameongoza harambee ya ununuzi wa kiwanja cha Parokia ya Mtakatifu Pius X Tarakea Jimbo katoliki Moshi.

Katika harambee hiyo kiasi cha Shilingi 82,841,900 kimepatikana ambapo ahadi ni Shilingi 36,313,000 na fedha taslimu zilizopatikaa ni Shilingi 46,528,900.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa harambee hiyo Waziri Mkenda amewapongeza waumini wote kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kujitolea kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kanisa.

Prof Mkenda amewahakikishia wananchi wa Rombo na waumini wa Parokia ya Mtakatifu Pius X Tarakea Jimbo katoliki Moshi kuwa ofisi ya mbunge itaendeleza ushirikiano kwa ajili ya shughuli zote za maendeleo ya kanisa.

Kadhalika, Waziri Mkenda ametoa rai kwa Kanisa kuendelea kushirikiana na serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wote.

About the author

mzalendoeditor