Featured Kitaifa

RAIS SAMIA :’WAKATI WA KUFATUTA WATOTO VIJANA WANAHANGAIKA NA SUPU YA PWEZA, VUMBI LA KONGO

Written by mzalendoeditor

Na Alex Sonna-DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameziagiza taasisi na Idara ya afya kufanya utafiti katika suala zima la lishe ili kuepuka kuwa na nguvu kazi isiyo imara kwa Taifa kwani vijana wamekuwa wakihangaika kutafuta supu ya Pweza na Vumbi la Mkongo

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Septemba 30,2022 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji Saini Mkataba wa usimamiaji wa  shughuli za lishe iliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Zanzibar ulioambatana na uzinduzi wa vifaa mbalimbali vya Afya ikiwemo Pikipiki na magari.

Rais Samia amesema kuwa vijana wenye umri balehe wamekuwa hawezi kuzalisha bila kutumia dawa za kuongeza nguvu.

Amesema  wakati wakutafuta watoto vijana hao wanahangaika mara kunywa supu ya pweza,vumbi la kongo na kwamba kuna tatizo ambalo wanalijua lakini hawalifanyii utafiti.

“Watafiti fanyeni tafiti, tuna tatizo, kwasababu halisemwi ni siri linawaumiza zaidi vijana wetu, mara haya ninayoyataja, mara vumbi la Kongo, mara kitu gani lakini ukifuatilia tatizo kubwa liko kwenye lishe,Sasa watafiti fanyeni tafiti vijana wetu waweze kuzaa watoto wenye afya ili Taifa liendelee kuwa Imara,”amesema.

Aidha amemuagiza Waziri wa Nchi – TAMISEMI kuwasilisha taarifa ya Halmashauri zote ambazo zimetumia fedha za lishe katika kutekeleza miradi mingine ili hatua kali ichukuliwe kwa wahusika.

Amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia fedha zinazopangwa kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya lishe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuhakikisha zinatolewa kwa wakati ili kutekeleza afua za lishe.

Amesema kuwa mpango wa lishe hautekelezwi ipasavyo, hivyo Wakuu wa Mikoa wahakikishe wanajipanga na kuongeza jitihada za kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za lishe bora na kupanga vipaombele ili kuleta tija

Aidha Rais Samia amesema kuwa Serikali itaweka nguvu zaidi kwenye uboreshaji wa huduma bora za afya katika Vituo vya Afya kwa kuwekeza kwenye ununuzi wa vifaa na vifaatiba, madawa, kuajiri watumishi pamoja na kujenga nyumba za watumishi.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Nassoro Ahmed Mazrui amesema kuwa lishe duni bado ni tatizo kubwa katika jamii hasa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na wanye umri wa kujifungua

“Mbali na jitihada zinazofanywa na Serikali yetu chini ya Rais Dkt.Mwinyi bado ni Nchi ambayo inakabiriwa na tatizo la lishe ikiwemo udumavu na utapiamlo mkali,ukosefu wa virutubisho mwilini,na Kuongezeka kwa maradhi yasiyoyakuambukiza Kutokana na ulaji usio sahihi,”amesema.

Naye Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameahidi kuandaa kutoa sera na miongozo ya kutoa huduma za lishe na kupitia Sera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili Mtumba kwa ajili ya kushiriki hafla ya uwekaji wa saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala pamoja na Watumishi wa Serikali mara baada ya kuweka saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika  leo Septemba 30,2022 jijini  Dodoma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa mara baada ya kuzindua mpango wa ugawaji wa magari pamoja na pikipiki yatakayotumika kwenye Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mtumba Mkoani humo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa magari pamoja na pikipiki yatakayotumika katika mpango wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mtumba Mkoani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua mabanda mbalimbali yanayohusiana na Sekta ya Afya na Lishe kabla ya kushiriki hafla ya uwekaji wa saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma 

Makatibu Tawala pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

Wakuu wa Mikoa wakiweka saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha moja ya mikataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe mara baada ya kuusaini katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

Wakuu wa Mikoa wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa saini mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe, Mtumba Jijini Dodoma 

 

About the author

mzalendoeditor