Featured Kitaifa

KASEKENYA AAGIZA TANROADS KUTENGENEZA MAENEO KOROFI

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza na Mameneja wa Mikoa pamoja na Wahandisi wakati akifungua  kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), nchini kilichoanza leo Septemba 24,2022 hadi 25 jijini Dodoma.

………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

MAMENEJA wa Wakala wa Barabara (TANROADS),nchini wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutengeneza maeneo korofi ya barabara na madaraja ili yaweze kupitika.

Agizo hilo limetolewa leo Septemba 24,2022 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Wakala huo.

Mhandisi Kasekenya amewataka kusimamia uendelezaji wa miundombinu kwa ufanisi mkubwa  ili kutoa mchango mkubwa kwa Taifa.

“Miundimbinu ya barabara ni kichocheo katika ukuzaji wa Sekta nyingine hivyo hakikisheni mnajenga na kukarabati maeneo yote korofi ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji”, amesema Mhandisi Kasekenya

Hata hivyo Mhandisi Kasekenya  ameagiza uongozi wa TANROADS kutoa elimu kwa wasafirishaji na wadau wote wanaotumia miundombinu ya barabara nchini kutomwaga mafuta, michanga, mawe na kokoto ambavyo vinapelekea kuharibu miundombinu hiyo.

Aidha amewataka Mameneja hao kuendelea kuwa wabunifu, waadilifu na kusimamia kazi zao kwa ubora na kwa wakati ili kuleta matokeo chanya yatakayopelekea Sekta ya Ujenzi kupiga hatua kubwa.

“Endeleeni kutumia utaalamu wenu katika ujenzi na usimamizi wa miradi ili kuwa na miundombinu bora itayokidhi mahitaji ya vizazi vya sasa na vijavyo”,amesisitiza Mhandisi  Kasekenya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Ujenzi, Balozi Mha. Aisha Amour,amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili na kushauri namna bora ya kutatua kero za watumiaji wa miundombinu ya barabara. 

“Kikao hiki kinalenga zaidi katika kazi za matengenezo ya barabara, miradi ya maendeleo inayoendelea, usalama barabarani na matukio ya ajali hivyo tumieni fursa hii kuleta mwazo chanya yatakayoikuza Sekta”, ameeleza Balozi Aisha.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Dar es Salaam, Eng. Haroun Senkuku, ameeleza kuwa ofisi yake inatarajia kuongeza barabara za juu (flyover) nyingine tatu (3) ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia na kutoka katika jiji hilo.

Naye, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Motta Kyando,amesema kuwa kazi za matengenezo ya barabara katika mkoa huo kwa mwaka wa fedha 2021/22 zimekamilika kwa asilimia 95 na kwa sasa hali ya barabara katika mkoa huo ni nzuri kwani inapitika majira yote ya mwaka.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akizungumza na Mameneja wa Mikoa pamoja na Wahandisi wakati akifungua  kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), nchini kilichoanza leo Septemba 24,2022 hadi 25 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya,akisisitiza jambo kwa washiriki (hawapo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), nchini kilichoanza leo Septemba 24 hadi 25,2022 jijini Dodoma.

KATIBU  Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Ujenzi), Balozi Mhandisi Aisha Amour, akitoa taarifa fupi katika kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta hiyo kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), nchini kilichoanza leo Septemba 24,2022 hadi 25 jijini Dodoma.

Baadhi ya Mameneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (hayupo pichani), wakati akifungua  kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), nchini kilichoanza leo Septemba 24,2022 hadi 25 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mara baada ya kufungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), nchini kilichoanza leo Septemba 24,2022 hadi 25 jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor