Featured Kitaifa

MAGENDO YAMTIA MATATANI AFISA UPELELEZI WILAYA YA MKINGA

Written by mzalendoeditor

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati wa  baada ya kikao chake katika kituo cha Polisi Chumbageni

……………………………….

Na Oscar Assenga,MKINGA

AFISA Upelelezi wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tanga kwa tuhuma za kudaiwa kushiriki kuwaachia  watuhumiwa 15 kati ya 20  licha ya kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kutokana na kushiriki vitendo vya uingizaji wa magendo yenye thamani ya Bilioni 1.2 ambao walikamatwa nayo nyakati tofauti  wa operesheni mbalimbali wilayani humo.
Licha ya kukamatwa lakini pia amesimamishwa kazi huku akimshukuru IGP Camilius Wambura kwa kutoa kibali cha kukamatwa kwa askari huyo naye ataingia kwenye mkondo wa sheria ili hali itendeke maana Jeshi la Polisi kazi yao  ni kukamata na baadae watawapeleka kwenye chombo vyengine vya kisheria ikiwemo mahakamani kama alivyosema Rais Samia kwamba mtu asionewe.
Katika operesheni hiyo walikamatwaa watuhumiwa 20,magari mawili na Mabeli ya vitenge 180  ikiwemo kwenye jahazi walikamata  watuhumiwa wanne na kuachiwa bila kufuata utaratibu wa kisheria kufanyika na hata hakukufunguliwa kesi wala jalada.
Akizungumza baada ya kikao chake katika kituo cha Polisi Chumbageni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema Afisa Upelelezi huyo wa wilaya ya Mkinga ameamua kuwaachia watu hao bila kufuata utaratibu
Akiwa wilayani Mkinga baada ya kutembelea mpaka wa Horohoro na Kituo cha Polisi wilayani Mkinga,RC Mgumba alisema kwamba amebaini kwamba watu waliokamatwa kwenye majahazi hayo wameachiwa huru na hawapo mahabusu wala Gereza lolote na hakuna mtu anayejua wapo wapi wakati kesi hiyo Rais Samia Suluhu anaijua,IGP Wambura anaijua  lakini Polisi Mkinga wamewaachia.
“Nilivyofika hapa wakati wa ziara yangu nilichokibaini kwamba Mzigo wote nimeukuta kwenye ghala la  TRA Mkinga na Ghala la Bandarini Tanga lakini kilichonisikitisha ni watu hao wameshtakiwa kwa uhujumu uchumi wapo watu wana miaka miwili  mitatu lakini hawa wamekamatwa na vithibitisho na wameachiwa kwa maelekezo ya nani hakuna mtu anayejua? Alihoji
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba lakini kamati ya ulinzi na usalama na RPC,Serikali wametoa maelekezo kwamba wakae lakini Polisi wa chini wameamua kuwaachia kwa maelekezo ya Afisa Upelelezi wilaya ya Mkinga kwa madai ya akieleza kwamba alipata maelekezo kwa Afisa Upelelezi Mkoa huu kwamba awaachie kwa sababu hayupo nilimuuliza swali moja kwamba Afisa Upelezi anaweza kitengua maelekezo ya RPC hakuna hivyo inaonyesha kwamba Jeshi hilo hawapo pamoja hawawezi kufanikiwa.
Alisema hayo yamefanyika kama Serikali wataendelea kufanyia kazi wanamshukuru IGP Wambura kwa ushirikiano wanaompa,RPC na wengine ombi lake waendelee kutoa ushirikiano huo huo wanamsaidia Rais Samia Suluhu ili maelekezo yake aliyoyatoa hadharani kwamba kipaumbele chake cha kwanza ni usalama wa mipaka,usalama wa raia na mali zao jambo la tatu ni mapato na matumizi ya mapato hayo.
“Kama mnavyojua kwamba Sasa tupo kwenye mjadala mpaka wa tozo Sasa kama kuna watu ambao hawajamuelewa Rais na kuachia mapato kuendelea kuvuja sidhani kama wanamsaidia ..hili nimelipokea kwa masikitiko makubwa kamati ya ulinzi na usalama tutakwenda kulijadili na tutawataarifu viongozi wetu wa juu kuhusu askari hao
Akieleza namna walivyokamata magendo hayo Mkuu huyo wa mkoa alisema Septemba 8 mwaka huu saa sita usiku walikamata jahazi likiwa limebeba beli la vitenge akiwa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa huo ambapo beli 170 zenye doti 17000 vipande vitatu vitatu vyenye zaidi ya Milioni 500.
Alisema pia Septemba 11 mwaka huu walikamata magari mawili aina ya fuso yaliyokuwa yamebeba beli a kila moja beli 90 za vitenge juu pamoja na mawe ya Tanga Stone ambapo beli hizo 180 jumla ya watu 20 ambapo kati yao wabebaji 14,wenye mizigo 2,madereva 2 na makondakta 2 hulu akieleza kwenye hilo jahazi walikamata watuhumiwa wanne dereva na Msaidizi wake baada ya hapo walipelekwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama.
Mkuu huyo wa mkoa alisema maelekezo ya Pili ni kwamba watumishi sheria ya Pili ya kuutaifisha mzigo na juzi walianza kufuatilia maagizo hayo kwamba  Serikali moja ya sheria zake zinger sheria zinazosimamiwa na TRA za kijinai,uhujumu uchumi wa nchi lengo kubwa ni kukomesha tabia za uvujaji wa mapato kwa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
“Nitoe onyo kwa wale wanaofanya biashara haramu msitarajie Kwamba itakuwa kama zamani waende kuongea wanamalizane badala yake watataifisha kwa kutumia sheria ya upande wa Pili kuitaifisha na sio kuwapa nafasi ya kulipa kodi mpaka atakapopata maelekezo mengine ngazi za juu”Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo  Maneja wa TRA Mkoa wa Tanga Speciaoza Owure alisema kwamba magendo hayo yalikamatwa Septemba 11 na yamehifadhiwa kwenye ghala lao la Horohoro wao wamepokea maagizo ya mkuu huyo wa mkoa na kusaidia kwenda kuyafanyia kazi kama mlivyosikia ambacho kimeamuliwa mgendo yanayokamatwa mkoa wa Tanga ni kuyataifisha na kuna sheria ya kulipwa faini na kodi ambayo ingepotea kwa sasa wataendelea kuitaifisha mpaka watapopata maelekezo mengine.
Owure alitoa wito kwa wafanyabiashara wafuate sheria na taratibu za kuingiza mizigo kwamba wajua magendo yana athari nyingi kwa  nchi wanaweza kuingiza vitu hatarishi na hazijapita kwa taratibu kwenye lengo kuingilia hivyo ni muhimu aidha zote zipite kwenye eneo ambalo lipo kisheria.
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu alisema kwamba wanamshukuru Mkuu huyo wa Mkoa amekwenda watapata maelekezo nini kifanyike baada ya kukamatwa kwa mzigo huo kwa siku tano zilizopita. 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati wa  baada ya kikao chake katika kituo cha Polisi Chumbageni

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akikagua bidhaa za magendo 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akikagua bidhaa za magendo 

 Na Oscar Assenga,MKINGA

AFISA Upelelezi wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tanga kwa tuhuma za kudaiwa kushiriki kuwaachia  watuhumiwa 15 kati ya 20  licha ya kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kutokana na kushiriki vitendo vya uingizaji wa magendo yenye thamani ya Bilioni 1.2 ambao walikamatwa nayo nyakati tofauti  wa operesheni mbalimbali wilayani humo.

About the author

mzalendoeditor