Featured Kitaifa

AJALI YAUA WATU SABA MANYARA, 14 WAJERUHIWA

Written by mzalendoeditor

Na John Walter-Manyara
Watu saba wamefariki dunia na wengine Kumi na nne  wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani baada ya  gari dogo la abiria  kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Cheka nao kata ya Kiperesa wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara  George Katabazi, amesema ajali hiyo imetokea Septemba 19 majira ya  saa 12:00 asubuhi ambapo watu sita walifariki papo hapo na mmoja alifariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda amesema gari hilo lenye namba za usajili T 266 APM aina ya Mitsubish Mini Bus linafanya safari zake Kutoka Matui Kiteto kwenda Kondoa mkoani Dodoma.
Katabazi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva  uliosababisha gari hilo kuhama njia na kupinduka ambapo baada ya tukio Dereva huyo aliejulikana kwa jina moja la Nurdin alikimbia.

About the author

mzalendoeditor