Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI DKT. DUGANGE, SERIKALI YATENGA SH.BILIONI .69.95 UNUNUZI WA VIFAA TIBA

Written by mzalendoeditor

Asila Twaha, OR- TAMISEMI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema, katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga Sh. Bilioni 69.95 kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma katika sekta ya afya ikiwemo uboreshaji wa huduma ya upatikanaji wa dawa, vitenganishi na vifaa tiba.

Akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Jacqueline Msongozi(Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma) alipotaka kujua
Lini Serikali itaboresha huduma za afya katika vituo vya afya ili huduma ziendelee kutolewa.

Mhe. Dugange amesema Serikali inaendelea kuboresha sekta ya afya katika uboreshaji wa huduma za upatikanaji wa dawa kwa kuongeza bajeti ya afya, kuendelea kuajiri watumishi sekta ya afya na kuwapeleka nchi nzima.

Pia amesema Serikali itaongeza bajeti ya ununuzi wa dawa kwa mwaka wa fedha uliopita na mwaka wa fedha 2022/23 na ununuzi vitenganishi na vifaa tiba.

“Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya nchini kote na vituo vyote vya afya 530 vilivyojengwa vitapatiwa vifaa tiba ili wananchi waweza kupata huduma bora”amesema Mhe. Dugange

About the author

mzalendoeditor