Featured Kitaifa

SERIKALI YAWATAKA VIONGOZI HANANG KUHIFADHI VYABZO VYA MAJI

Written by mzalendoeditor

Serikali imetoa wito kwa viongozi wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara kuendelea kuhamasisha wananchi kuhifadhi vyanzo vya maji ikiwemo maziwa ya Bassuto na Ziwa Eyasi.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni jijini Dodoma leo Septemba 14, 2022.

Mbunge wa Hanang Mhe. Samweli Xaday alitaka kufahamu mpango gani wa kufanya utafiti wa kujua sababu za kusambaa kwa maji ya Ziwa Bassuto na Kuhama kwa samaki kwenye Ziwa Eyasi.

Mhe. Khamis alisema kwa sasa Serikali imeona hakuna haja ya kufanya utafiti wa kujua sababu ya kusambaa kwa maji na kuhama kwa samaki katika Ziwa Bassuto. 

Akiendelea kuibu swali hilo alifafanua kuwa sababu kuu ni kujaa maji wakati wa mvua nyingi, ziwa hilo ni dogo halina uwezo wa kuhifadhi maji mengi yanayosababishwa na mvua nyingi.

“Mhe. Spika maji hayo yanapojaa ziwani humo hutawanyika na kuingia kwenye Ziwa Eyasi na kwa kuwa Ziwa Bassuto lina viumbe mbalimbali ikiwemo samaki, maji hayo yanapoingia kwenye Ziwa Eyasi huingiza na viumbe mbalimbali wanaoishi kwenye Ziwa Bassuto ikiwemo samaki,” alisema.

Hivyo Naibu Waziri Khamis alisema hali hiyo inasababisha wananchi wanaotegemea samaki wa Ziwa Basuto inawabidi kupata samaki hao kwenye Ziwa Eyasi.

About the author

mzalendoeditor