Featured Kitaifa

WAZIRI BASHUNGWA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA RC KAGERA

Written by mzalendoeditor

OR -TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa Kagera, Mhe. Albert John Chalamila kuunda Tume maalum itakayopokea malalamiko ya ardhi yaliyokidhiri katika Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkoani Kagera.

Ametoa agizo hilo leo tarehe 10 Septemba 2022 wakati aliposhiriki kikao cha Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilaya karagwe na kupokea malalamiko ya kuibuka vna kukithiri kwa migogoro sugu ya ardhi bndani ya wilaya ya Karagwe.

Amesema Tume hiyo maalum itafanya kazi ya kufuatilia kwa undani migogoro sugu na inayoendelea kuibuka ndani ya mkoa Kagera ambayo inachangia uvunjifu wa amani na kuleta umasikini kwa wananchi.

Aidha, Bashungwa amepokea changamoto kuhusu vijana wasiokuwa na Vitambulisho vya NIDA kutopewa Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ambapo Bashungwa amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambayo ipo katika mfumo Mpya wa utoaji wa Mikopo katika Halmashauri.

HBashungwa amesema kutokana na changamoto ya upatikanaji wa Vitambulisho vya NIDA katika mikoa ya mipakani, Ofisi ya Rais TAMISEMI itafanya Maboresho ya mfumo huo ili kutoa fursa kwa vijana ambao hawajapata vitambulisho hivyo kunufaika na mikopo hiyo.

Wakati huo, Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi Kubwa anayoifanya ya kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais kwa fedha nyingi za miradi anazoendelea Kuleta Mkoa Kagera.

About the author

mzalendoeditor