Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATAKA USHIRIKI WA WATOTO KATIKA MABARAZA YAO

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum  Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa kumkabidhi bendera ya Taifa Mtoto Victor Paschal Tantau anayetarajiwa kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Watoto Duniani utakaofanyika nchini Denmark kuanzia tarehe 13 hadi 16 Septemba, 2022.

……………………..

Na WMJWM, Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi nchini kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwenye Mabaraza ya watoto yaliyopo katika ngazi za Kata hadi Taifa kwani katika mabaraza hayo ndipo vipaji vya watoto hao vinajengwa

Akitoa Salamu za Rais Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum M. Doirothy Gwajima wakati wa kumkabidhi bendera ya Taifa Mtoto Victor Paschal Tantau anayetarajiwa kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Watoto Duniani utakaofanyika nchini Denmark kuanzia tarehe 13 hadi 16 Septemba, 2022.

Amesema kuwa Watoto wanastahili haki ya kushiriki na kushirikishwa kwenye masuala yanayowahusu. ikiwa ni kutekeleza Haki hiyo ya Msingi kwao na inayotambuliwa na Baraza la Usalama la Umoja la Umoja wa Mataifa likihusisha viongozi wa nchi wanachama wa Umoja huo kwenye mkutano maalum iliofanyika tarehe 8 hadi 10 Mei, 2002 ikiwa na maazimio kadhaa likiwemo azimio la kuunda chombo maalum kwa ajili ya ushiriki na ushirikishwaji wa Watoto katika masuala yanayowahusu.

Amefafanua katika kutekeleza azimio hilo, mwezi Desemba 2002 Serikali iliunda Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwezesha Watoto kukutana na kujadili masuala yanayohusu haki, ulinzi na maendeleo yao kwa ujumla.

Pia Waziri Dkt Gwajima amesema katika kuimarisha ushirikishwaji wa Watoto , Serikali iliandaa Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya Mwaka 2008 na kwenye Sura ya 5 imetoa maelekezo kwa wadau kuhakikisha kuwa Watoto wanashirikishwa kunapo masuala yanayowahusu.

“Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 inatambua kwamba mtoto anapaswa kushirikishwa masuala yanayomhusu” alisema Waziri Dkt. Gwajima

Aidha Waziri Dkt. Gwajima, ameeleza kuwa Mabaraza ya watoto ndio msingi wa kuwajenga watoto kupitia klabu za watoto shuleni ambazo ndio nguzo za utendaji wa mabaraza ya watoto nchini hivyo Klabu hizo za watoto zinatumiwa na wawezeshaji wa watoto kujadili masuala mahsusi yanayohusu watoto yakijumuisha; Uongozi, Uzalendo kwa Taifa lao na Maadili Mema.

Naye Mtoto Victor Paschal Tantau amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Wizara inayosimamia masuala ya ustawi wa mtoto na kumuomba kuendelea kuwasaidia watoto ambao hawana uwezo wa kupata haki zao za msingi hasa Elimu.

“Nasema asante sana Mhe. Rais, Mhe. Waziri na viongkzi wote wa Wizara hii kwa kutupa fursa watoto ili tuweze kuonesha na kujenga vipaji vyetu tulivyonavyo kwa manufaa ya ustawi wetu” alisema Mtoto Victor

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto Sebastian Kitiku amesema Serikali kupitia Wizara inayosimamia masuala ya Maendeleo ya Mtoto itahakikisha inaratibu uanzishiwaji na uendeshaji wa Mabaraza ya watoto nchini ili yaweze kusaidia kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuvumbua vipaji vya watoto na kuviendeleza kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo Baba wa mtoto huyo Paschal Tantau amesema Mabaraza ya watoto yana uwezo mkubwa wa kuwajengea watoto kuweza kujiamini na kuvumbua vipaji vyao kwani hadi kufikia hatua ya Mtoto wake Victor kuchaguliwa kushiriki Mkutano huo wa Kimataifa ni Baraza la Watoto la Mkoa ndio limemjengea uwezo Mtoto wake mpaka kufikia hatua hiyo.

Mtoto Victor Paschal Tantau anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Watoto Duniani utakaofanyika nchini Denmark kuanzia tarehe 13 hadi 16 Septemba, 2022.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum  Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa kumkabidhi bendera ya Taifa Mtoto Victor Paschal Tantau anayetarajiwa kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Watoto Duniani utakaofanyika nchini Denmark kuanzia tarehe 13 hadi 16 Septemba, 2022.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima  akimvisha bendera ya Taifa Mtoto Victor Paschal Tantau anayetarajiwa kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Watoto Duniani utakaofanyika nchini Denmark kuanzia tarehe 13 hadi 16 Septemba, 2022.

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na Mtoto Victor Paschal Tantau na wazazi wake anayetarajiwa kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Watoto Duniani utakaofanyika nchini Denmark kuanzia tarehe 13 hadi 16 Septemba, 2022.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJWM

About the author

mzalendoeditor