WANACHAMA nane wamepitishwa na chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Ubunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) utakaofanyika Septemba 22,2022.
Akitangaza majina hayo yaliyopitishwa na Kamati ya Wabunge wa CCM leo Septemba 10,2022 jijini Dodoma Msimamizi wa uchaguzi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amewataja waliochaguliwa kuwa ni Nadra Juma Mohamed, Dk.Abdulla Hasnuu Makame, Machano Ali Machono.
Wengine ni Angela Kizigha, Dk.Shogo Mlozi, James Ole Millya, Dk.Ng’waru Maghembe na Anar Kachambwa.
Uchaguzi wa wajumbe tisa watakoiwakilisha Tanzania EALA utafanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake utakaoanza Septemba 13, mwaka huu.