Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YARIDHISHWA NA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA TAEC KIKOMBO JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

KAMATI ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii,ikipata maelezo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),iliyopo Kikombo jijini Dodoma leo Septemba 8,2022.

………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

KAMATI ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeridhishwa na ujenzi wa makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),iliyopo Kikombo jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa maabara na ofisi za taasisi hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Nyongo,ameipongeza serikali kwa kufanikisha ujenzi huo.

Mhe.Nyongo amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kwa kupima mionzi kwenye bidhaa zao kwa usalama wa nchi kwani itahudumia maeneo mengi ikiwamo ya kusini mwa Tanzania, Kigoma, Iringa, Mbeya na maeneo ya mipakani.

“Hii tume ina kazi kubwa sana ya kudhibiti mionzi na kuzuia matumizi mabaya ya mionzi kwenye chakula, simu kwa kuwa matumizi mabaya yanaweza kusababisha madhara.”amesema Nyongo

Hata hivyo amesema kuwa  kamati imeridhishwa na thamani ya fedha ambao mkandarasi amelipwa asilimia 50 lakini ujenzi upo asilimia 85 na linagharimu Sh.Bilioni 3.8.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda, amesema kuwa huduma zinazotolewa na Tume hiyo zitaanza kutolewa mwaka huu kwenye makao makuu hayo.

”Tume hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya kisayansi kwenye nyuklia , usalama katika vifaa vya Hospitali vinavyotumia mionzi na chakula.”amesema Prof.Mkenda

Prof.Mkenda ameeleza kuwa serikali itaendelea kuwaendeleza wanasayansi katika masuala ya nyuklia.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Prof.Lazaro Busagala, amesema kujwa ujenzi huo unahusisha maabara na ofisi za taasisi hiyo pindi itakapohamisha makao yake Dodoma.

“Kujengwa kwa Ofisi hii tutaokoa gharama nyingi za uendeshaji na utawala ambazo zinasababishwa na umbali wa makao makuu ya taasisi ambayo kwasasa yapo Arusha,”amesema.

KAMATI ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii,ikipata maelezo mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),iliyopo Kikombo jijini Dodoma leo Septemba 8,2022.

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa makao makuu ya Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),yanayojengwa Kikombo jijini Dodoma leo Septemba 8,2022.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii  kutembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa taasisi hiyo inayojengwa Kikombo jijini Dodoma leo Septemba 8,2022.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),Prof.Lazaro Busagala,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii  kutembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa taasisi hiyo inayojengwa Kikombo jijini Dodoma leo Septemba 8,2022.

MUONEKANO wa jengo la Tume ya Nguvu za Atomiki(TAEC),linalojengwa Kikombo jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor