Featured Kitaifa

MADEREVA BODABODA JIJINI MBEYA WAPEWA ELIMU YA USALAMA BARABARANI.

Written by mzalendoeditor

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewataka madereva wa Pikipiki za magurudumu mawili maarufu bodaboda kutii sheria bila shuruti kwa kuhakikisha wanafuata na kuheshimu sheria za usalama barabarani.

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Mbeya ACP ABDI ISSANGO ameyasema hayo Septemba 05, 2022 katika uwanja wa FFU Jijini Mbeya wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Bodaboda wa Jiji la Mbeya.

ACP Issango amewataka Bodaboda kutojihusisha na uhalifu wa aina yoyote iwe ni kwa kubeba mali za wizi au kusafirisha wahalifu na badala yake amewataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Mrakibu wa Polisi Yussuf Kamotta [RTO] amekemea tabia ya baadhi ya madereva wa Bodaboda ya kuendesha Pikipiki bila kuvaa kofia ngumu, kubeba abiria Zaidi ya mmoja na kupita kwenye taa za kuongozea magari bila kuruhusiwa. 

Imetolewa na,

ULRICH O. MATEI – SACP

Kamanda wa Polisi,

Mkoa wa Mbeya.

About the author

mzalendoeditor