Featured Michezo

TWIGA STARS YAANZA VYEMA KOMBE LA COSAFA

Written by mzalendoeditor

MABINGWA watetezi, Tanzania wameanza vyema michuano ya COSAFA kwa wanawake baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Comoro leo Uwanja wa Madibaz mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.
Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na Donisia Minja dakika ya 13 na Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ mawili dakika ya 41 na 52.
Baada ya mechi hiyo, nyota wa Twiga Stars Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ alipewa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa soka nzuri aliyoonyesha huku akitoa mchango mkubwa kwa ushindi wa timu yake kutokana na kufunga mara mbili.

About the author

mzalendoeditor