Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI KATIKA KISOMO CHA DUA KUMUOMBEA MAREHEMU KAKA YAKE HASSAN ALI HASSAN MWINYI

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakiongoza kisoma cha hitma kumuombea Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi, kilichofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jana usiku 2-9-2022, na )kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh.Abubakar Zuberi.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakishiriki katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Sadala Mabodi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kupokea mkono wa pole kutoka kwa Wananchi mbalimbali waliohudhiria Kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea Marehemu Kaka yake Hassan Ali Hassan Mwinyi, kilichofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jana usiku 2-9-2022.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor