Featured Kitaifa

WAJASIRIAMALI WANAWAKE WAIOMBA SERIKALI KUPITISHA SERA MAALUMU KUTAMBUA JITIHADA ZAO

Written by mzalendoeditor

 Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Lindam Limited inayohusika na Mradi wa waendeleze kwa ajili ya kuwakuza Wanawake katika kilimo biashara Bi.Zuhura Muro ,akizungumza na Mzalendo Blog leo Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.

………………………….

Na Eva Godwin-DODOMA 

WAJASIRIAMALI Wanawake wameiomba Serikali Kupitisha Sera Maalumu kwa ajili ya kutambua Jitihada mbalimbali zinazotokana na uzalishaji mdogo mdogo wa majumbani ikiwa ni pamoja na kuendeleza Jukumu la kuangalia Familia pamoja na kuchangia katika pato la Taifa.

 Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Lindam Limited inayohusika na Mradi wa waendeleze kwa ajili ya kuwakuza Wanawake katika kilimo biashara Bi.Zuhura Muro ,akizungumza na Mzalendo Blog leo Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma

Amesema shughuli nyingi za kina mama ambao wanazalisha mnyororo wa Kilimo na mifugo wanazalishia Majumbani na hakuna Sera maalumu ambayo imepitishwa na Serikali inayoshighulika na Viwanda vya nyumbani.

” Nchi kama Indonesia, China, Malaysia  zimetambua Sera ambayo Mwanamke anaweza kuanzisha kiwanda kidogo chenye mitambo ambayo sio mikubwa sana akaendesha kiwanda chake palepale kwenye nyumba yake na huku anaendelea kulea Watoto”, amesema

“Kwa hiyo Mama akitengenezewa Sera ya kuweza kuangalia kwamba Sera inaweza kulinda viwanda majumbani itkuwa imemsaidia Mama mjasiriamali na pia itaongeza pato la Taifa letu”. Amesema  Bi.Muro

Naye  Mkurugenzi wa Pima General Interprises Limited iliyopo Mkoani Kagera inayojihusisha  na utengenezaji sabuni za kuogea na za chooni kwa kutumia mchikichi Bi.Pili Makunenge ,amesema shughuli hiyo amejitenfenezea kiwanda chake nyumbani kwake na pia kuwaajiri baadhi ya kina Mama kushirikiana katika shughuli hiyo.

” Mimi nazalishia bidhaa zangu nyumbani na namshukuru Mungu mambo yanenda huku nikishirikiana na Lindam Limited katika mradi wake wa Waendeleze Women in agree business na tangu nikishirikiana na Lindam nimepata Fursa mbalimbali ikiwemo elimu ya kuweza kutunza kumbukumbu katika bidhaa zangu ikiwa pia elimu ya kutengeneza sabuni na Watu wenye utaalamu mkubwa kutengeneza sabuni

“Kwasasa uzalishaji wa sabuni umeongezeka kwasababu nimekuwa nikishirikiana na kampuni mbalimbali katika kupata vitu tofauti vya kunisaidia kutengeneza bidhaa zenye ubora zaidi”.Amesema Makunenge

 Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya Lindam Limited inayohusika na Mradi wa waendeleze kwa ajili ya kuwakuza Wanawake katika kilimo biashara Bi.Zuhura Muro ,akizungumza na Mzalendo Blog leo Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Pima General Interprises Limited iliyopo Mkoani Kagera inayojihusisha  na utengenezaji sabuni za kuogea na za chooni kwa kutumia mchikichi Bi.Pili Makunenge ,akizungumza na Mzalendo Blog leo Agosti 31, 2022 Jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor