Featured Kitaifa

DC MBONEKO : SHINYANGA TUMEJIPANGA VIZURI KUFANIKISHA KAMPENI YA CHANJO YA POLIO

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amesema wilaya hiyo wamejipanga kikamilifu kufanikisha Kampeni ya Chanjo ya Polio kwa awamu ya tatu kuanzia Septemba 1 hadi 4 ,2022 itakayofanyika nyumba kwa nyumba kwa watoto wote walio chini ya miaka mitano.

Mboneko ameyasema hayo wakati wa kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu kilichofanyika leo Jumatano Agosti 31,2022 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
 
“Awamu hii ya tatu tunategemea matokeo yatakuwa makubwa zaidi baada ya kufanya vizuri kwenye awamu ya pili iliyopita ambapo tulikuwa wa kwanza. Huu ugonjwa ni mbaya, maradhi haya siyo ya masihara hivyo ni lazima watoto wapate chanjo ,Watoto wakipata chanjo watakua vizuri, wataepuka magonjwa”,amesema Mboneko.
 
“Katika Kampeni hii ya awamu ya tatu malengo tuliyojiwekea ya walengwa 88,376 kwa Halmashauri ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga 44,013 isipungue, tusikie namba imeongezeka, tuwafikie watoto wote, wawepo wataalamu wa kutosha na kwenye maeneo ambayo kuna changamoto wataalamu waongezwe”,amesema Mboneko.
 
Mkuu huyo wa wilaya amesisitiza watoto wapate chanjo hiyo ya matone hata kama walipata chanjo kwenye awamu ya pili kwa ajili ya kuwakinga na ugonjwa wa Polio.
 
“Chanjo ya Polio inaanza Septemba 1 hadi 4 kwa watoto wote walio chini ya miaka mitano. Hii ni chanjo ya matone siyo chanjo ya sindano na chanjo hii ni salama haina madhara.
 
 Zoezi hili ni la kitaifa, Mtu atakayepotosha sheria zipo , ukipotosha tutakuchukulia hatua”,ameongeza Mboneko.
 
Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Immaculate Dotto amesema lengo la Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu ni kuongeza uelewa kwa wanajamii kuhusu faida za Chanjo ya Polio na katika awamu hii  kampeni itafanyika kwa siku nne kuanzia Septemba 1 hadi 4,2022.
 
“Naomba viongozi na wanajamii waendelee kutoa elimu kuhusu Polio na kuhamasisha watoto wote wapate chanjo ya Polio. Ugonjwa huu unasababishwa na Virusi vya Polio vinavyosababisha kupooza na hatimaye kifo. 
 
Virusi hivi huingia mwilini kwa njia yam domo,kwa kunywa maji au chakula kilichochafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa virusi hivyo. Ugonjwa huu hauna tiba lakini unaweza kuzuiliwa tu kwa kupata chanjo ya matone ya polio”,amesema Dotto.
 
Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Shinyanga, John Alphonce Sakwa amesema walengwa wa kampeni ya chanjo ya Polio katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ni watoto 88,376 na Manispaa ya Shinyanga 44,013 huku akieleza kuwa Chanjo itafanyika nyumba kwa nyumba na itaendelea kutolewa pia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
 
 
“Sambamba na uchanjaji huduma zingine zitatolewa ikiwemo elimu ya chanjo kwa jamii, kuimarisha huduma za chanjo katika vituo vya kutolea chanjo pamoja na kuwatafuta na kuwafuatilia watoto wote wenye umri chini ya miaka 15 ambao wamepata ulemavu ghafla tepetepe (washukiwa wa ugonjwa polio) na kutoa taarifa vituo vya karibu kwa uchunguzi na kubaini ugonjwa huu wa polio”,amesema Sakwa.
 
 
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga David Rwazo wamesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafanikisha vizuri kampeni hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na takwimu sahihi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4, 2022. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Immaculate Dotto akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga David Rwazo akizungumza kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Shinyanga, John Alphonce Sakwa akiwasilisha taarifa kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Wadau wakiwa kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022
Wadau wakiwa kwenye Kikao cha kamati ya afya Wilaya ya Shinyanga kuhusu Kampeni ya Chanjo ya Polio awamu ya tatu itakayofanyika kuanzia Septemba 1 – 4,2022.
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
 

About the author

mzalendoeditor