Featured Kitaifa

WANAHARAKATI, WANAHABARI NA WASANII BARA LA AFRIKA WAMEKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZINAZOZUIA MAENDELEO YA WAAFRIKA.

Written by mzalendoeditor
………………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Vuguvugu la wanaharakati,wanahabari, na wasanii Afrika zaidi ya 700 wamekutana mkoani Arusha katika mkutano wa All African movement Assembly (AAMA) kwaajili  kujadili changamoto mbalimbali zinazozuia maendeleo ya waafrika.
Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo mjumbe wa bodi ya African Rising ambao ndio waandaaji wa mkutano huo  Mwalimu Mutemi Wakiama alisema kuwa wamewaleta pamoja waafrika ili waweze kujadiliana kuhusu mambo ya mbeleni ya Afrika, kwa kuangalia mambo ambayo yameshafanyika, mahali walipo, wapi wanaenda na yapi ambayo yanatakiwa kurekebishwa ili waweze kuwa na Afrika huru.
“Tunayaangalia haya ili tuweze kuwa na Afrika ambayo inawasaidia waafrika wajisikie kama binadamu ambao wamekombolewa kutoka ukoloni mambo leo ambapo mojawapo ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na magonjwa elimu, mabadiliko ya tabia ya nchi, Haki ya Mwanamke,Haki ya Kiuchumi na Utu kwa waafrika, Nafasi ya kijamii, ulinzi wa wanaharakati, uhamiaji na itikadi za Kiafrika zisizo na mipaka, Utamaduni wa Kiafrika siku zijazo pamoja na uhuru wa kujieleza,” Alisema.
Kwa upande wao baadhi washiriki wa mkutano huo  Maimuna Asraji  mkurugenzi wa shirika la Mendacious better cost organization ya nchini Kenya alisema kuwa lengo la wao kufika katika mkutano huo ni kuona ni kwa namna gani wao kama waafrika wataweza kuwa na mshikamano na kuondokana na changamoto ambazo zinaleta vikwazo katika kuingia na kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.
“Tunataka kuona sisi kama vijana wa Afrika mashariki wanaposema umoja wetu ndio nguvu yetu katika wimbo wa EAC iwe hivyo na sio kutuvunja moyo tunapifika mipaka, Kuna maswali mengi yanavunja moyo, lakini pia tunachangamoto kwa upande wa elimu kijana akitokea Tanzania, Kenya, Uganda aua Bukinafaso kuweza kusoma Kuna mambo mengi anapitia,” Alisema.
Alieleza kuwa wanajadili masuala hayo ili kuweza kuja na suluhu lakini pia kuona ni vipi waafrika wataweza kujisimamia wenyewe katika elimu, Afya, kwa katika masuala mbalimbali yanayoikumba dunia Afrika inatetemeka zaidi  na kuitisha msaada katika mabara mengine japo ina nchi tajiri zaidi pale inapokumbwa na majanga kama ya njaa na magonjwa ndio maana wamejumuika kuona ni jinsi gani tunatatua changamoto zinazowakumba.
Joseph Nazareth kijana kutoka nchini Kenya alisema wamekuja kutafuta njia ya kutatua changamoto zinazowakumba kama  bara la Afrika na kama vijana na ni matumaini yake wakitoka katika mkutano huo na kurudi katika mataifa yao wataanza vuguvugu la kuandaa na kuwakilisha miswada na mapendekezo kwa viongozi wao katika serikali zao tofautitofauti moja ikiwa ni kuwa na Afrika huru isiyo na mipaka wala vizuizi kutoka eneo moja kwenda lingine.
“Tunataka tuwe na uhuru wa kibiashara kwa kuruhisiwa kufanya biashara bila vizuizi na vikwazo na iwe rahisi kupata hati za kusafiria  kwani hii itasaidia kujenga bara letu lakini pia kuona ni namna gani nchi zilizopiga hatua katika demokrasia na siasa zinaweza kusaidia nchi nyingine katika kujikuza na kujipanua kidemokrasi na kisiasa,” Alisema Nazareth.
Naye Vincent Uhega kutoka voice of youth Tanzania alisema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na kutokuwa na pesa moja kama bara jambo linalopelekea mtu anapopita katika nchi moja kwenda nchi nyingine kubadilisha fedha nyingi  lakini wakiwa na pesa moja yenye nguvu kama mabara mengine itasaidia kutembea kwa haraka na kufanya biashara kwaajili ya maendeleo ya bara zima.
“Unatoka Tanzania ulifika Kenya unabadisha pesa, ukifika South Sudan unabadisha tena hivyo  hivyo kwa kila nchi utakayoingia lakini pia thamani ya pesa inashuka kulinga na thamani ya pesa ya nchi nyingine na hii inafanya wafanyabiashara wengi kushindwa kuwekeza kibiashara katika nchi zingine za Afrika, tusiwe wabinafsi na kuacha mazungumzo yetu kwenye makaratasi tufanye kama zilivyofanya nchi za ulaya,” Alisema.
Vincent Uhega kutoka voice of youth Tanzania akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wa All African movement Assembly unaoendelea mkoani Arusha.
 Mshiriki wa mkutano wa All African movement Assembly Joseph Nazareth kijana kutoka nchini Kenya akiongea na waandishi wa habari katika katika mkutano huo.
Maimuna Asraji  mkurugenzi wa shirika la Mendacious better cost organization ya nchini Kenya akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo unaoendelea mkoani Arusha
baBaadhi ya washiriki wa mkutano wa All African movement Assembly wakifuatilia jambo katika mkutano huo unaoendelea mkoani Arusha.
Mjumbe wa bodi ya African Rising ambao ndio waandaaji wa mkutano huo  Mwalimu Mutemi Wakiama akiongea na waandishi wa habari.

About the author

mzalendoeditor