Featured Michezo

STARS YAPASUKA KWA MKAPA,NJIA PANDA KUFUZU CHAN 2023

Written by mzalendoeditor

 

Na Alex Sonna

TIMU ya Taifa Stars imejiweka njia panda kufuzu Michuani ya Wachezaji wa ndani CHAN mashindano yatakayofanyika nchini Algeria 2023 baada ya kuchapwa bao 1-0 na Uganda mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa  jijini Dar es Salaam.

Akitokea benchi Mshambuliaji Travis Mutyaba aliwanyamazisha Watanzania waliohudhuria mechi hiyo dakika ya 87 baada ya kuchachafya ngome ya Taifa Stars.

Tanzania inahitaji kwenda kupindua meza ugenini mnamo tarehe 3 Septembar mwaka huu katika uwanja wa St.Mary nchini Uganda timu hizo zitarudiana mshindi wa Jumla atafuzu moja kwa moja kuelekea nchini Algeria 2023

About the author

mzalendoeditor