WAMEDHAMIRIA ndivyo unavyoweza kusema! Timu ya Arsenal imeendeleza Moto na haishikiki baada ya kutoka nyuma na kupata ushindi wa nne mfululizo wakiichapa mabao 2-1 Fulham FC mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Stadium Jijijni London.
Mabao ya Arsenal yamefungwa Martin Odegaard dakika ya 56 na Gabriel Magalhaes dakika ya 85, wakati la Fulham limefungwa na Aleksandar Mitrović dakika ya 56.
The Gunners wanafikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi zote nne na sasa wanaongoza Ligi kwa pointi mbili zaidi ya Manchester City.