Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Wajumbe wa Shrika la Maendeleo D,tree kuhusiana na uimarishaji wa Wahudumu wa Afya wa Kujitolea CHV, walipofika Ofisini kwake Mnazimmoja kujadili maendeleo ya wahudumu hao.
………………………………
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema wataendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya maendeleo ili kuimarisha sekta ya afya nchini.
Akizungumza na washirika wa maendeleo ya afya D,Tree huko Ofisini kwake Mnzimmoja mara baada ya kufika na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu wahudumu wa Afya ya kujitolea (CHV), amesema wahudumu hao ni muhimu sana kwani wanaisaidia Wizara katika kuendesha harakati mbalimbali za Kiafya.
Amesema wahudumu wa afya wa kujitolea (CHV ) wanafanya kazi ngumu na kubwa katika jamii ikiwemo kuwapatia elimu ya kuimarisha Afya ya mama na mtoto jambo linaloisaidia Wizara katika kupunguza madhara yatokanayo na uzazi.
Aidha amefahamisha kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha kuwa inaimarisha maslahi ya wahudumu hao ili kuwapa moyo Zaidi wa kuendelea kufanya kazi na kuhakikisha Afya za jamii zinaimarika .
“Baadhi ya wanajamii hawana uwelewa kuhusu maendeleo ya afya ya uzazi ambapo mama mjamzito huchelewa kufika hospitali na kusababisha ongezeko la vifo vya mama na mtoto,hivyo wahudumu hawa wanajukumu kubwa la kutoa elimu zaid kwa jamii.”alisema Waziri Mazrui
Nao wajumbe wa Shirika la D,Tree wameishukuru Wizara ya afya kwa ushirikiano wao na kuahidi kuongeza ushirikiano Zaidi katika sekta hiyo ili kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza . Wakati huohuo Waziri Mazrui alikutana na ujumbe kutoka Uturuki na kujadili kuhusu upatikanaji wa madawa na vifaa tiba ambavyo vitasaidia katika matibabu mbalimbali kwa wagonjwa.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi zawadi maalum Mjumbe wa Shrika la Maendeleo Dtree mara baada ya kujadili uimarishaji wa Wahudumu wa Afya wa Kujitolea CHV huko Wizarani kwake Mnazimmja Zanzibar.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Wajumbe wa Shrika la Maendeleo D,tree kuhusiana na uimarishaji wa Wahudumu wa Afya wa Kujitolea CHV, walipofika Ofisini kwake Mnazimmoja kujadili maendeleo ya wahudumu hao