WAZIRI wa maji Jumaa Aweso akiongea na wananchi katika uzinduzi wa mradi wa ondoshaji mchanga katika njia ya mto Nduruma Arusha.
………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka wakuu wa mabonde yote 9 ya maji kuhakikisha wanainisha na kuvitambua vyanzo vyao maji na kuviwekea mipaka mapema na sio kusubiri wananchi waanze kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa vyanzo ndipo waende na kuathiri shughuli hizo.
Aweso ameyasema hayo wakati akizinduzi mradi wa kuondoa mchanga mto nduruma ili kuurudisha katika mkondo wake wa asili ambapo alisema kuwa pamoja na wakuu hao kuvitambua na kuweka mipaka pia washirikishe taasisi nyingine katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na wananchi na sio kukaa maofisini na kusubiri waziri aende au uharibifu ufanyike ndipo waibuke.
“Sio mwananchi anakuja anapanda mahindi yake yanakuwa wewe ndo unakuja na panga lako kuyakata, ulikuwa wapi mkuu wa bonde?, nawasisitiza msilete taharuki kwa wananchi, jamii siku zote ipo mkiishirikisha mtafanikiwa na msipo ishirikisha mtakwama,” Alisema Aweso.
Alisisitiza kuwa ni lazima kushirikisha jamii zilizozunguka vyanzo vya maji kwani ndio msingi wa kwanza wa kuleta mafanikio katika ulindaji na utunzaji wa maji lakini pia wakubali kufanya kazi na wadau wakiwemo maafisa mazingira na misitu wa halmashauri na mikoa.
Sambamba na hayo pia Waziri Aweso amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuongeza shilingi milioni miamoja katika mradi huo huku akiwaelekeza bonde la maji kutoa mifuko mia moja kwaajili ya maendeleo ya wananchi katika Halmashauri ya meru.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango aliwapongeza wananchi kwa kuacha eneo hilo kwaajili ya kuchimba mtaro huo ili kuurudisha mto kwenye njia yake Hali itayowasaidia kuondoka na majanga mbalimbali ikiwemo mafuriko kuingia katika makazi na mazao kuharibiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bonde la maji mto pangani Segule Segule ambaye anatekeleza mradi huo amewashukuru wananchi pamoja na viongozi wa seikali ambao wanashirikiana katika kutunza vyanzo vya maji.
Diwani wa kata ya Shambaraiburka John Eliyau Mollel amesema kuwa athari za mto huo zimekuwa zikisababisha madhara makubwa kwa wananchi ikiwemo kupoteza maisha kutokana na mafuriko wakati wa Mvua.
Awali akisoma taarifa za mradi huo mtaalamu wa maji juu ya ardhi wa bonde la pangani Brown Mwangoka alisema kuwa mradi huo unakadiriwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 250 ambapo kwa mpango wa muda mfupi unakadiriwa kutumia milioni 100 na hadi Sasa wameshatumia milioni 80 kwa kilometa 3.5.
Alieleza kuwa mradi huo utondoa atha ya mafuriko ya mara kwa mara katika makazi ya watu takribani 730 pmoja na kuokoa mashamba ekari 3280 ambayo yalikuwa yakiathiriwa na mafuriko pamoja na kupunguza gharama za ukarabadi na ujenzi wa barabara.
WAZIRI wa maji Jumaa Aweso akiongea na wananchi katika uzinduzi wa mradi wa ondoshaji mchanga katika njia ya mto Nduruma Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru John Danielson akiongea katika uzinduzi wa mradi huo katika kata ya Shambaraiburka Wilayani Arumeru.
MKURUGENZI wa bodi ya maji ya bonde la mto pangani mhandisi Segule Segule akiongea katika uzinduzi huo.
BAADHI ya wananchi wa kata ya Shambaraiburka Wilayani Arumeru wakifuatilia jambo katika uzinduzi wa mradi wa ondoshaji mchanga katika njia ya Mto Nduruma.
WAZIRI wa maji Jumaa Aweso akiongea mara baada ya kuzindua mradi wa ondoshaji mchanga katika njia ya mto Nduruma katika kata ya Shambaraiburka.
WAZIRI wa maji Jumaa Aweso akikagua eneo liliondoshwa mchanga kwaajili ya urejeshwaji wa njia ya asili ya mto Nduruma.
WAZIRI wa maji Jumaa Aweso akizindua mradi wa ondoshaji mchanga katika njia ya mto Nduruma uliopo chini ya bodi ya maji ya bonde la mto Pangani.