WADAU mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,wakati akifunga Mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi Cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ulioandaliwa na Wizara hiyo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma.
……………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imewataka Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini kuongeza machapisho ya tafiti katika majarida makubwa duniani ili waweze kutambulika ulimwenguni kama watafiti wabobezi.
Hayo yamesemwa leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda wakati akifunga Mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi Cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ulioandaliwa na Wizara hiyo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo Agosti 25,2022 jijini Dodoma.
Prof.Mkenda amesema kuwa kwa sasa wahadhiri wengi wanaogopa sana kufanya tafiti hasa zile za kisayansi.
“Hatutaweza kwenda kwenye maeneo yote kwa wakati mmoja tunataka tuanze na utafiti wa elimu tiba,sasa hivi watu wanaogopa kufanya utafiti wa muda mrefu kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo kwa kulitatua hilo tumetenga bilioni Moja ambapo Kila mtafiti atakayekidhi vigezo atapata Shilingi milioni 50,”amesema Mkenda
Prof.Mkenda amesema ulimwengu wa sasa hauwezi kuepukana na masuala ya sayansi na Teknolojia hivyo kutaka wadau wote kuchochea udadisi na ubunifu kwa watoto ili baadae waweze kuajirika na kujiajiri.
“Tunataka kuvutia vijana wenye uwezo mkubwa wasome masomo ya sayansi na ili tufanikiwe katika hilo lazima tuwekeze katika elimu kwa kufuata misingi ya sayansi,ubunifu na Teknolojia,”amesisitiza Mkenda
Hata hivyo Prof.Mkenda amesema kuwa wizara hiyo ipo mbioni kutambulisha mpango wa ufadhili wa masomo wa “Samia Scholarship”kwa wanafunzi bora 600 waliofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi.
“Tutatangaza hivi karibuni kitu kinachoitwa SAMIA SCHOLARSHIP kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vizuri masomo ya sayansi katika kidato cha sita na kwenda kusoma masomo hayo chuo kikuu; lengo ni kuongeza idadi ya vijana watakaopenda kusoma masomo ya sayansi,” amesema Prof. Mkenda.
Aidha Waziri Mkenda amelishukuru Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuwezesha kufanyika mkutano huo huku akiwataka wadau walioshiriki kikao na wasioshiriki kuendelea kutoa maoni kupitia majukwaa yatakayowekwa.
“Nitoe wito hata kwa wale ambao hawapo hapa kuendelea kutoa maoni kupitia platforms zitakazowekwa. Tunapenda tukishaweka Sera basi idumu isibadilishwe mara kwa mara na tunaahidi kuzingatia maoni yenu yote mliyotoa na ambayo mtaendelea kuyatoa,” amesema Waziri Mkenda.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Aloyce Kamamba ameiomba serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuyafanyia kazi maoni ya wadau pamoja na kuzichukua,kuzitambua,kuzifadhili na kuziendeleza bunifu zinazobuniwa.
Pia amesema kuwa mawazo yaliyotolewa na wadau yasibakie katika makaratasi yafanyiwe kazi ili kutatua changamoto zilizopo katika jamii kupitia Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
” Sera hizi zisibakie tu kuwa zimeandikwa kwenye makaratasi kwani mkutano huu wa wadau utakuwa umefanyika bure kwani lengo kubwa ni kutaka kuona ni namna gani sayansi,teknolojia na ubunifu inakwenda kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii,”Amesema Kimamba
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula, amesema kuwa wamepokea maoni kutoka kwa wadau kuhusiana na kuhuisha rasimu ya Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi Cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ulioandaliwa na Wizara hiyo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma.
WADAU mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,wakati akifunga Mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi Cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ulioandaliwa na Wizara hiyo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula,akielezea malengo ya Mkutano huo wakati wa Mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi Cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ulioandaliwa na Wizara hiyo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Aloyce Kamamba,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi Cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ulioandaliwa na Wizara hiyo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa wadau wa kupokea maoni kuhusu Sera ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na Kiunzi Cha Uratibu wa Ubunifu nchini,ulioandaliwa na Wizara hiyo, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) leo Agosti 26,2022 jijini Dodoma.