Featured Kitaifa

SERIKALI YATOA BILIONI 15 KUNUNUA MAGARI POLISI

Written by mzalendoeditor

Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 15 kwa ajili ya kununua magari yatakayo pelekwa kwa Makamanda wa Polisi wa mikoa na kwa Ma Ocd pamoja na fedha ya mafuta itakayokwenda moja kwa moja wilayani ili kurahisisha utendaji kazi za Polisi.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya Polisi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amewataka askari wahitimu kuwaheshimu Watanzania ikiwa pamoja na kutenda haki sambamba na kuyashughulikia matukio ya uhalifu kwa wakati na kwa haraka.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura amesema kuwa hadi sasa hali ya nchi ni salama na ina amani na utulivu wa kutosha ikiwa bado Jeshi hilo linaendelea kudumisha hali hiyo kwa kushirikiana na wananchi, vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya utoaji haki.

Kwa upande wake Mkuu  wa Shule ya Polisi Tanzania SACP Ramadhani Mungi amesema shule ilipokea zaidi ya wanafunzi 4310 na waliohitimu mafunzo hayo 4122 huku wengine 186 wakiachishwa  mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu.

Aidha, wahitumu hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya nadharia na vitendo.

About the author

mzalendoeditor