Burudani Featured

MAANDALIZI YA TAMASHA LA SENSABIKA YAKAMILIKA,WASANII ZAIDI YA 70 KUNOGESHA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiongea na waandishi wa habari jjini Dodoma Agosti 20, 2022, kuhusu Tamasha la Sensabika ambalo litafanyika Agosti 21, 2022 katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam kuwahamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika nchini 

………………………………..

Na Eleuteri Mangi, WUSM

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema maandalizi ya Tamasha la Sensabika yamekamika na litafanyika Agosti 21, 2022 katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jjini Dodoma Agosti 20, 2022, Dkt. Abbasi amesema tamasha hilo limebuniwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa lengo la kuwaleta watu pamoja na kuwahamashisha watu wote kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Mkazi ifikapo Agosti 23, 2022.

“Tamasha la Sensabika limekuja kuhakikisha kila Mtanzania anayepswa kuhesabiwa anahesabiwa ili kujua kuna watu wangapi kwenye kaya, ni takwimu ambazo zikienda kuchakatwa zitaisaidia Serikali kujua eneo fulani kuna watu wangapi tuwapelekee huduma gani” amesema Dkt. Abbasi.

Dkt. Abbasi ameongeza kuwa Kampeni ya Sensabika ilianza kwa upande wa mitandaoni na kutangazwa wiki moja iliyopita kuwa Jumapili Agosti 21, 2022 saa kadhaa kabla ya Sensa Agosti 23, 2022 tamasha hilo kubwa la Sensa litawaleta Watanzania pamoja.

Tamasha la Sensabika litapambwa na wasanii zaidi ya 70 na watapanda jukwaani kuwahamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ambapo nyimbo zitaimbwa pamoja na michezo mbalimbali itachezwa kuanzia asubuhi hadi usiku.

Tamasha litaanza kwa kukimbia mchakamchaka pamoja na kutembea kuanzia Coco beach hadi leaders Club ambapo washiriki wote watafanya mazoezi mepesi, yoga, michezo ya jadi, mchezo wa ngumi, kuvuta Kamba pamoja na mashindano ya kukimbiza kitoweo  

About the author

mzalendoeditor