Na Odilo Bolgas
SIMBA wameendelea kuwasha moto katika mechi za Ligi baada ya kuichapa kagera Sugar mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji Mosses Phiri amezidi kuonyesha uimara wa kucheka na nyavu baada ya kuiandikia Simba bao dakika ya 42.
Kipindi cha pili Simba walipata bao la pili likifungwa na Mshambuliaji kutoka Serbia Dejan Georgijevic dakika ya 81.
Kwa ushindi huo Simba wanaendelea kukaa kileleni wakiwa na Pointi 6 sawa na Yanga huku wao wakiwa na mabao matano ya kufunga na wakiwa hawajaruhusu bao lolote.