Featured Kitaifa

AAMA KUWAKUTANISHA WANAHARAKATI, WASANII, WAANDISHI WA HABARI ZAIDI YA 1000 KUTOKA BARA ZIMA LA AFRIKA, MKOANI  ARUSHA 

Written by mzalendoeditor
NA  NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Zaidi  ya watu 1000 kutoka bara zima la Afrika na Dispora wanatarajiwa kukutana mkoa wa Arusha katika katika mkutano wa All African movement Assembly (AAMA) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayotia wasiwasi kama vile usalama, mifumo ya Afya iliyoharibika, Rushwa, mabadiliko ya tabia ya nchi, utawala bora na mengineyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na mshauri wa vyombo vya habari kutoka African Rising Ann Lorna amesema kuwa mkutano huo utafanyika Agosti 29 hadi 31 mwaka huu ambapo pamoja na majadiliano hayo pia kutakuwa na mazungumzo ya mseto yatakayokuwa na lengo la kujenga mamlaka katika mashina ili kuifanya Afrika kuwa kubwa.
Alifafanua kuwa pia kutakuwa na jukwaa la  mashauriano ya kikanda ambayo ni fursa pekee ya  uhamasishaji wa kuimarisha hali ya sasa ya kuandaa Pan African katika bara zima ambapo mashauriano hayo ni muhimu kwani yatajenga mshikamano miongoni mwa waafrika wanaohisika na afya na ustawi wa jumuiya zao za ndani na Afrika kwa ujumla.
Alisema majukwaa ya wanachama wao yana lengo la kuonyesha kazi zao za uanaharakati kuhusu masuala ya haki ya kijinsia, mabadiliko ya tabia ya nchi, utawala bora, usawa na utu, na nafasi ya  kiraia ambapo mawasilisho kutoka katika mashauriano mbalimbali yataandaliwa na kushirikishwa kwenye  mkutano huo na wanatarajia kuwa mwenyeji washiriki zaidi 750 wanaojumuisha vuguvugu, wanaharakati, wasanii, waandishi wa habari, asasi za kiraia na kuendelea.
“Wakati ambapo ukosefu wa usalama unaongezeka katika maeneo mengi ya Afrika na nchi kadhaa za Afrika zinaelekea katika uchaguzi, kumekuwa na ongezeko la rushwa iliyokithiri  lakini pia  kuna haja kubwa ya ubunifu  katika ufumbuzi wa huduma za afya, tunataka kusikia kutoka kwa wanachama wetu kote Afrika ni  jinsi wanavyosimama ili kukidhi mahitaji na changamoto za jumuiya zao katika siku hizi,” Alieleza Ann Lorna.
Aliendelea kueleza kuwa  miongoni mwa maeneo yatakayozingatiwa ni jinsi ya kujenga mshikamano kwa ajili ya vuguvugu zenye nguvu katika bara zima ili kusaidia katika kujenga Afrika wanayoitaka ikiwa ni pamoja na kuanzisha uhusiano wa msingi katika nchi mbalimbali na kuweza kutengeneza mpango endelevu 
Hata hivyo Africans Rising taayari wameshafanya mikutano 5 ya kikanda katika Afrika ya Kati, Magharibi, Kusini, Mashariki na Kaskazini.

About the author

mzalendoeditor