Featured Michezo

SIMBA YAANZA NA MOTO LIGI KUU,YAISHUSHA YANGA

Written by mzalendoeditor

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mabingwa wa zamani  Simba wameanza na moto kwenye ligi ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi Geita Gold, mchezo uliopigwa  katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo ambao ulionekana wa aina yake hasa kwa timu zote kuonesha soka safi la kushambulia kutafuta mabao.

Shangwe ziende kwa wachezaji wapya wa timu ya Simba ambapo leo wameonesha makali yao kwa kucheza kandanda safi na wengine kupachika mabao safi, mabao ya Simbaa yaliwekwa kimyani na Augustino Okrah ambaye lipiga free kick ambayo ilimshindinda kipa kwa Geita Gold na kutinga nyavuni.

Mpaka mapumziko Simba Sc ilikuwa mbele kwa bao 1-0,na baadae mshambuliaji wao mpya Moses Phiri kupachika bao kali ambalo liliwanyanyua mashabiki kwa furaha kwenye dimbaa la Benjamini Mkapa.

Simba Sc ilipata bao la tatu kupitia kwa kiungo wao mshambuliaji Clautos Chama ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati namatokeo kusomeka Simba Sc kuibuka na Ushindi wa mnono wa 3-0.

Kwa ushindi huo Simba wamekamata usukani wa Ligi wakiwa na pointi tatu sawa na mabingwa Yanga huku Simba wakiwana uwiano mzuri wa magoli.

About the author

mzalendoeditor